KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 6, 2009

MTAZAMO WA UFISADI KATIKA DINI





UFISADI

MTAZAMO WA UFISADI KATIKA DINI

QURAN AND BIBLIA

UFISADI KATIKA MTAZAMO WA DINI, NI JAMBO AMBALO LINA MSINGI WA MABAYA YOTE. UFISADI NI JENGO LA UKOSEFU WA HURUMA NA HAKI, KATIKA JAMII. UFISADI JENGO LAKE HALINA JINSIA.

(DUME AU JIKE).

MWENYEZI MUNGU ANASEMA KATIKA KITABU KITAKATIFU CHA QURAN:

“WANAVUNJA AHADI YA MWENYEZI MUNGU, BAADA YA KUIFUNGA NA KUYAKATA ALIYOAMRISHA MWENYEZI MUNGU KUUNGWA NA KUFANYA KATIKA ARDHI. HAO NDIO WENYE KHASARA”.
(2: 27)

KUVUNJA AHADI YA MWENYEZI MUNGU KUNAWEZA KUSABABISHA MAAFA KATIKA JAMII NA KUPATA ADHABU KUTOKA KWA MWENYEZI MUNGU.

MFANO:

KUAPA KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU YA KWAMBA, UTAKUWA MKWELI NA MWAMINIFU KATIKA KAZI ULIOPEWA UTAKUWA TAYARI UMEMFANYA MWENYEZI MUNGU SHAHIDI. IKIWA UTAVUNJA SHERIA ZA KIAPO HUSIKA, TAYARI UMEVUNJA AHADI YA MWENYEZI MUNGU, NA KWENDA KINYUME NA AHADI YA KIAPO CHAKO. JAMII ITAKUSHUHUDIA KWA MAKINI NA IKICHUNGUZA UTEKELEZAJI WA KAZI ZAKO, IKIWA UTAENDA KINYUME NA MAKUBALIANO YA AHADI, JAMII ITAKUWA NI YENYE KUKULAUMU KUTOKANA NA KUVUNJIKA KWA AHADI.

MWENYEZI MUNGU ANAAMRISHA HAKI NA KUKATAZA DHULUMA, IKIWA UTAWADHULUMU WATU, TAYARI UNAINGIZWA KATIKA KUNDI LA MAFISADI. KILA FISADI ANA HASARA KATIKA ARDHI. ATAISHI KATIKA MASHAKA, UKOSEFU WA RAHA, LAANA …….N.K

BIBLIA:
MAANDIKO YA BIBLIA YANATUFAHAMISHA HAYA KUHUSU UFISADI:

KWA SABABU MWILI HUTAMANI UKISHINDANA NA ROHO, NA ROHO KUSHINDANA NA MWILI, KWA MAANA HIZI ZIMEPINGANA , HATA HAMWEZI KUFANYA MNAYOTAKA. LAKINI MKIONGOZWA NA ROHO, HAMPO CHINI YA SHERIA. BASI MATENDO YA MWILI NI DHAHIRI, NDIO HAYA.


UASHERATI - UCHAFU - UFISADI - UZUSHI – IBAADA YA SANAMU - UCHAWI – UADUI – UGOMVI – WIVU – HASIRA – FITINA - FARAKA – UZUSHI – HUSUDA – ULEVI – ULAFI – NA MAMBO YANAYOFANANA NA HAYO; KATIKA HAYO NAWAAMBIA MAPEMA, KAMA NILIVYOKWISHA KUWAAMBIA, YA KWAMBA WATU WATENDAO MAMBO YA JINSI HIYO HAWATAURITHI UFALME WA MUNGU.

(WAGALATIA 5: 17…..21)

KATIKA MTAZAMO WA BIBLIA, TUNAONYESHWA VITA BAINA YA ROHO NA MWILI. MWILI HAUWEZI KUWEPO BILA ROHO NA BINAADAMU HAWEZI KUISHI DUNIANI BILA MWILI.

KUMBUKA YA KWAMBA MUUNGANO WA ROHO NA MWILI NI NAFSI. NAFSI NI CHOMBO AMBACHO KINAONGOZA MWILI KATIKA SHUGHULI ZOTE ZA MAISHA. MWISHO WA MAISHA NAFSI INAKUFA ( MWILI UNATENGANA NA ROHO ) KISHA MWILI HUOZA LA KINI ROHO HAIFI, KINACHO KUFA NI MUUNGANO BAINA YA MWILI NA ROHO NAO NI NAFSI.

NAFSI INAWEZA KUMPELEKA MHUSIKA PABAYA BILA KUJUA. NI VYEMA KILA NAFSI KUEPUKANA NA HARAMU NA KUFUATA HALALI. IKIWA UNAPENDA KUTENDEWA HAKI KWA NINI UWANYIME WATU WENGINE HAKI ZAO. MUNGU AMEKUAHIDI MAUMIVU DUNIANI NA MWISHO WA YOTE UTATUPWA KATIKA JAHANAMU (MOTO).

No comments:

Post a Comment