KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 6, 2009

HAKI NI KIFAA CHENYE THAMANI YA UADILIFU






A.W.W. B.R.R.

HAKI NI KIFAA CHENYE UBORA NA THAMANI KAMA YA UADILIFU. UADILIFU NI KUWEKA KITU SEHEMU YAKE BILA YA UPENDELEO.

KATIKA NYUMBA YA HAKI HUWEZI KUKUTA MALALAMIKO, KUSONONEKA, LAWAMA ,WIVU ,MATUSI , UMWAGIKAHI WA DAMU ZISIZO NA HATIA, UASHERATI, CHUKI, FITNA, MAJUNGU, HUSDA………..N.K. KILA BINAADAMU ANACHUKIA JAMBO AMBALO NI BAYA KWAKE, NA ANAPENDA ATENDEWE VIZURI NA AAMBIWE MANENO MAZURI.

LAKINI JAMBO LAMSINGI LA KUJIULIZA NI KWAMBA, IKIWA UNAPENDA KUTENDEWA MEMA AU KUAMBIWA MANENO MAZURI, JE ! WEWE UNATENDA HAYO?

EBU TUANGALIE MUONGOZO ( QURAN NA BIBLIA ) WA MWENYEZI MUNGU UNATUELEKEZA VIPI ?

QURAN:

NA ILI WAJUE WALE WALIOPEWA ILIMU YA KWAMBA HIYO NI HAKI ILIYOTOKA KWA MOLA WAKO NA WAIAMINI, ILI ZINYENYEKEE KWAKE NYOYO ZAO. NA KWA YAKINI MWENYEZI MUNGU NDIE AWAONGOZAYE WALE WALIOAMINI KATIKA NJIA ILIONYOKA.
( 22 : 54 )

MWENYEZI MUNGU ANATUELIMISHA KUHUSU KUFUATA HAKI, NA KWAMBA HAKI INATOKA KWAKE. KUMBUKA YA KWAMBA DHULMA NITAMU ZAIDI YA HAKI JUU YA NYOYO ZA MADHALIMU, LAKINI KWA UPANDE MWINGINE WA WALE WENYE NYOYO ZINAZOMTII MWENYEZI MUNGU, HUWA NA CHUKI JUU YA DHULMA NA KURIDHIKA NA HALI HALISI YAKIPATO CHAKE CHA UADILIFU. TUNAONA YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU NDIE ANAEWAONGOZA WAJA WAKE KATIKA NJIA YA HAKI ( ILIONYOOKA ).

QURAN : NA WATAENDELEA WALE WALIOKUFURU KUWA KATIKA WASI WASI KWA HILO ( ULIOKUJA NALO ) MPAKA KIAMA KIWAJIE KWA GHAFLA, AU IWAJIE ADHABU YA SIKU ISIYOKUWA NA KHERI
( NAO HATA KIDOGO ) ( 22 : 55 )

WATU WALIO KUFURU NI WALE WANAOBADILISHA HARAMU KUWA HALALI NA HALALI KUWA HARAMU, KUTOKANA NA MASLAHI YA NAFSI ZAO. WATU HAO HAWAJALI KUMWAGA DAMU, DHULMA, HUSDA, FITNA, LAWAMA, UDHALIMU, UONGO, UGOMVI………..N.K.
IKIWA ATAJITOKEZA MTU AU MCHAMUNGU KUPIGA VITA HARAMU NDANI YA NAFSI YAKE , ATAKUTANA NA VIKWAZO VYA KILA AINA NDANI YA MOYO. MOYO UNACHUKUWA NA FASI KUBWA KATIKA KUSHAWISHI AU KUONGOZA NAFSI YAKE KATIKA MAMBO MABAYA. NA NDIO MAANA MWENYEZI MUNGU KATAJA ILIMU. ILIMU NDIO ITAKAYO MFANYA AU KUFANYA NAFSI IWE NA UVUMILIVU AU LA JUU YA JAMBO HUSIKA.

KWA MAANA HII, WALIOKUFURU NI WATU WENYE JESHI KUBWA LA KUFRU NA HUWA NA MIKAKATI YA KUANGAMIZA KILA MWENYE KUSIMAMA NA BENDERA YA HAKI. UKITAJA HAKI WALE WALIOKUFURU WANAKUONA KAMA MTU MWENYE MADHARA JUU YA MASLAHI YA NAFSI ZAO. NA NDIO MAANA KUNDI HILO LITATUMIA KILA NJIA YA PESA AU MANENO, ILIMLADI WA KUANGAMIZE AU WAANGAMIZE HAKI.

BIBLIA


YESU “SIKUJA KUWAITA WENYE HAKI, BALI WENYE DHAMBI.

(MARKO 2: 17)

TUNAONA YA KWAMBA MTU MWENYE BENDERA YA HAKI NI MSAFI. HATA WATUKUFU WA MUNGU WALIPOKUJA ( KUTUMWA ) KUWAOKOA WATU DUNIANI, HAWAJAJA KWA SABABU YA WATU WENYE HAKI LA BALI WAMEKUJA KWASABABU YA WATU WENYE KWENDA KINYUME NA HAKI ( MADHALIMU AU WADHULMAJI )

BIBLIA

KWA MAANA HAKI YA MUNGU INADHIHIRISHWA NDANI YAKE, TOKA IMANI HATA IMANI; KAMA ILIVYOANDIKWA , MWENYE HAKI ATAISHI KWA IMANI. KWA MAANA GHADHABU YA MUNGU IMEDHIHIRISHWA KUTOKA MBINGUNI JUU YA UASI WOTE NA UOVU WA WANADAMU WAIPINGAO KWELI KWA UOVU.

( WARUMI 1 : 17…18 )

KWA MUJIBU WA MAANDIKO, TUNAONA YA KWAMBA KILAJAMBO MWENYEZI MUNGU AMELIWEKA WAZI NA AKAONESHA ( MUNGU ) UHALALI NA UHARAMU WA JAMBO HUSIKA, LAKINI BAADHI WA BINAADAMU WAMECHUKUWA JUKUMU LAKUBADILISHA UOVU KUWA UKWELI.

No comments:

Post a Comment