AJALI YA MORNING BUS
WILAYA YA RUFIJI MKOA WA PWANI
SEHEMU YA AJALI NI LUHOI
NAMBA YA GARI: T 674 ADY
SABABU YA AJALI: BREKI
MAJERUHI: WATU 30 MUNGU AWABORESHEE AFYA ZAO.
VIFO VYA WATU: WATU 8 MUNGU AWAWEKE MAHALA PEMA PEPONI.
HOSPITAL ZILIZO TUMIKA: SONGA NA HOI KIDOGO.
INASEMEKANA GARI, LILIPOTEZA BREKI KATIKA USAWA WA Km 3. KONDA ALIWEZA KURUKA ,KUTOKA NDANI YA MORNING BUS NA KUTUWA ARDHINI NA AKAWA SALAMA. ALICHOKIFANYA TANIBOI, YEYE ALIVYOONA HAKUNA MATUMAINI YA GARI KUPATA BREKI,ALIPENYA BAINA YA VITI ( KATIKATI YA MSITARI WA VITI NDANI YA BASI ) AKAKA CHINI NA KISHA AKATAFUTA SAPOTI YA KUMFANYA AWEZE KUHIMILI KISHINDO CHA MUANGUKO WA BASI. KILICHOTOKEA BAADAE,ABIRIA WOTE WALIKUWA NA HOFU KUBWA,WAKIWA NA MATUMAINI MADOGO JUU YA NAFSI ZAO KUENDELEA KUWA HAI.
BAADA YA BASI KUANGUKA,DEREVA ALITOKA NDANI YA BASI AKAWEZA KUMWOKOA MTOTO WA MIAKA MIWILI,ALIMTOA DIRISHANI AKIWA ANALIA KWA AJILI YA MAUMIVU. KILICHOTOKEA BAADA YA DEREVA KUMWOKOA MTOTO HUYO ALIMWEKA PEMBENI, KISHA AKAKIMBIA AKATOKA SEHEMU YA AJALI.
WATU WALIFIKA KWENYE TUKIO AKIWEMO KONDA WA KAANZA KUTOA MSAADA NDIPO WALIPOWAPATA MAJERAHA 30 NA MAITI 8.
KATIKA MAITI HIZO, KUNA DADA AMBAE JINA
MSIBA HUO ULIWAJAZA WATANZANIA WOTE MACHUNGU PAMOJA NAWAPENDA AMANI DUNIANI. ULIKUWA PIGO KUBWA JUU YA TARAFA NZIMA YA MKONGO.
KATIKA NDUGU ZETU WALIOPOTEZA MAISHA YAO ALIKUWEMO SHEIKH ABDALLAH NZORONGWA , AMBAYE KATIKA AJALI ALIKUWA AMEKAA NA MJUKU WAKE,AMBAYE ALITOKA SALAMA WALA HAKUUMIA.
SHEIKH ABDALLAH NZORONGWA, ALIKUWA NI KIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU, KATIKA KIJIJI CHA MLOKA.
SHEIKH NZORONGWA AMEACHA WAKE WA TATU ( 3 ) NA WATOTO ZAIDI YA SABA.
UMRI WA SHEIKH NZORONGWA NI ZAIDI YA MIAKA SITINI
(OVER 60 YEARS)
SIFA ZA SHEIKH NZORONGWA : ALIKUWA MNYENYEKEVU,AKITATUWA MATATIZO YA WANAKIJIJI BILA KUBAGUA RANGI,KABILA,DINI, SEHEMU, TAJIRI AU MASIKINI NA CHEO.
MUNGU WA MBINGU NA ARDHI,TUNAKUOMBA KWA UWEZO WAKO WA MILELE NA MILELE, UZIWEKE ROHO ZA WAJAWAKO KATIKA MAPUMZIKO YA AMANI NA UTULIVU. KILA JAMBO UNALIJUA VIZURI NA AMALI NJEMA WEWE NDIE MWENYE KUZITAMBUA, NAFASI YA KUSAMEHE AU KUADHIBU UNAYO WEWE PEKE YAKO. SISI BINAADAMU UMETUUMBA NA UKATUAHIDI KWAMBA KWAKO TUTAREJEA, WAZAZI WETU,NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WANAREJEA KILA KUKICHA TUKISHUHUDIA. EWE MUNGU TUNAKUOMBA UTUNUSURU NA MATENDO MABAYA HAPA DUNIANI KWA KUTUONGOZA KATIKA NJIA ILIONYOOKA KAMA ULIVYOWAONGOZA WACHAMUNGU WALIOPITA.
TUNAKUOMBA UWAWEKE MAHALA PEMA PEPONI, WAZAZI WETU, NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI WALIOTUTANGULIA.
AMINA
No comments:
Post a Comment