KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, March 29, 2009

MANENO NA VITENDO NDIO MSINGI WA HESHIMA YAKO



MAISHANI MNA SIRI MBILI,ZA MSINGI.

SIRI HIZO NI :

1) MANENO

2) MATENDO

SIRI HIZO NDIO MSINGI WA MAISHANI. ILI BINAADAMU AWEZE KUENDESHA MAISHA YAKE, YA KILA SIKU LAZIMA ATUMIE
SILAHA HIZO ( MANENO NA VITENDO ). MANENO NA VITENDO, NI VIFAA VIZURI VINAPOKUWA NA CHANZO KIZURI NA VINAWEZA KUWA SUMU AU VIBAYA VINAPOKUWA NA CHANZO KIBAYA
.

KILA BINADAMU ( NAFSI ) ANA UWEZO WA KUTENGENEZA
MANENO NA VITENDO VYA KIPEKEE.


TAFAUTI YA MANENO NA VITENDO INAWEZA KUJITOKEZA PALE,AMBAPO NAFSI YA MTU HUSIKA,INAWEZA KUNENA JAMBO FULANI NA ISIWEZE KULITEKELEZA, KUTOKANA NA UDHAIFU WAKE AU UPUNGUFU WA MILIKI ( MALI,MDA……..Etc ) AU UPUNGUFU WA ELIMU KUHUSU NENO LILILOTAMKWA NA NAFSI HUSIKA.

MANENO NA VITENDO NDIVYO VYANZO,VYA KUONESHA SURA AU MUONEKANO WA NAFSI HUSIKA. HEKIMA YA MTU HUTOKANA AU INAONEKANA KUKANA NA VITE NDO NA MANENO YAKE.

HII NDIO SIRI YA MANENO NA VITENDO , MAISHANI MWETU.
NIVYEMA UKITOA ,AHADI UITEKELEZE.
ILI UJENGE HESHIMA YAKO NA KUHESHIMIWA.
JARIBU KUFIKIRI,KUHUSU MANENO YA AHADI ULIOPEWA NA WATU,WAKASHINDWA KUKUTEKELEZEA AHADI HIO ?
ULIJIHISIJE MOYONO MWAKO ?
BILASHAKA ULICHUKIA NA KUPOTEZA ASILIMIA FULANI YA UAMINIFU,JUU YA YULE MUAHIDI.
WANGAPI UMEWATENDEA MABAYA, NA UNAJIHISI VIPI JUU YA UBAYA HUO ?
AU WALIOKUTENDEA MABAYA UNAWAHISI VIPI JUU YA UBAYA HUSIKA ?
KWA KWELI JIBU UNALO,MWENYEWE. TAFAKARI KISHA TUPE MAONI NA MSIMAMO WAKO, KUHUSU MANENO NA VITENDO.

No comments:

Post a Comment