KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 13, 2012

Mohammed Morsy ametangaza kuwa anamuondoa waziri wa ulinzi na mkuu wa jeshi

Nchini Misri, rais mpya, Mohammed Morsy
ametangaza kuwa anamuondoa waziri wa ulinzi na mkuu wa jeshi, Hussein Tantawi pamoja na naibu wake.
Rais piya amesema anafuta mabadiliko ambayo yalilipa jeshi madaraka zaidi. Mabadiliko hayo yasiyotarajiwa kuhusu majenerali wawili wakuu wa Misri, yalitangazwa na msemaji wa rais kwenye mkutano na waandishi wa habari uliotangazwa moja kwa moja kwenye televisheni. Field Marshal Tantawi,
ambaye alishika madaraka ya uongozi baada ya Rais Hosni Mubarak kuondoshwa madarakani mwaka jana, analazimishwa kustaafu pamoja na mpambe wake. Waziri mpya wa ulinzi ni jenerali mwandamizi, Abdel Fattah al-Sissi. Mabadiliko ya katiba ambayo yalitangazwa na jeshi wakati uchaguzi wa rais unafanywa mwezi wa Juni, piya yamefutwa. Lengo la mabadiliko hayo yalikuwa kupunguza madaraka ya rais. Bwana Morsy amekuwa kwenye vuta nkuvute na jeshi tangu ameshika madaraka. Ni wazi kuwa hatua yake hii ni jaribio la kuchukua uamuzi mkubwa.

No comments:

Post a Comment