KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, August 20, 2011

Dhuluma maishani




Wanawake wengi hujikuta katika hali ambayo wamedhulumiwa; kihisia, nyumbani, na kijinsia. Usione haya ukijikuta katika hali hii kwa maana kuna watu wengi sana wanaopitia hali moja sawa na yako. Ukipata usaidizi mapema ni vizuri. Bonyeza kwenye vivukio vifuatavyo ili upate maelezo zaidi.
Dhuluma ya kujamiiana


Ni hali ya kujamiiana ambayo inatokea bila hiari ya mtu. Una haki ya kusema ‘hapana’. Wanaodhulumu ni pamoja na watu wasiowajua, marafiki au jamaa. Hali ambapo watu wa baadhi ya familia moja wanapofanya tendo la ndoa bila ya ndoa namaranyingine niharamu kikabila au kimila au kidini namaranyingine wanapokutana kimapenzi baadhi ya watu huwaita ‘najisi’.

Dhuluma hizi ni pamoja na kunajisi, kushikashika, kumtesa mtu kwa maneno makali, hata kumlazimisha kuona picha au filamu chafu chafu. Wakati mwingine unakubali tu kwa sababu umeogopa au unaona maisha yako yakiwa hatarini.


Unaweza kukubali na pia uwe na mhasiriwa na dhulumwa za kingono.

Hakuna mtu aliye na haki ya kukushika, kuongea nawe maneno yanayohusu ngono, kukufanya utazame filamu chafu chafu za ngono au picha; ama hata kushiriki ngono ya mdomoni, utuputupu wa nyuma au ya utupu wa mbele iwapo hautaki. Kuna makundi yanayoweza kukusaidia iwapo umenajisiwa yatahakikisha kuwa haki zako zimetunzwa.


Maishani: Dhuluma inaweza kutumika katika njia nyingi zisizokuwa za kihalali. Uhalali wajambo unatokana na uwezo, ubora au utendaji wa jambo husika. Kila maamuzi yana historia. Kutokana na njia ya Ukosefu, upungufu au mchujo wa uhalisia wa picha(kitendo, msemo au ishara) husika.kwamaana hii basi utakosa umakini wakutambua maana na uhalisia wakile au yule uishi nae au yule ndugu yako ama yule rafiki yako bila kumsahau jamaa zako. Jambo zuri lakuepusha dhuluma ni uadilifu na kuishi bila kusahau muongozo wa uvumilivu na kujifunza kusamehe maishani.




Unapaswa kufanya nini iwapo umenajisiwa au kudhulumiwa kimapenzi?
Ukidhulumiwa kimapenzi, mpigie simu polisi au mtu yeyote wa kifamilia unayeweza kumwamini. Askari hawatakulazimisha kuchukua hatua lakini watakusaidia.

Usioge ama kusugua meno. Andika chini maelezo ya kila namna uliyodhulumiwa na aliyekudhulumu. Inaweza kuwa vigumu lakini ni muhimu na inahitajika kwa ushahidi.


Hakikisha kuwa polisi wanakupeleka kwanza kwenye kliniki, hospitali au kwa daktari wa upasuaji; omba kifuko cha walionajisiwa na ukaguliwe iwapo umeambukizwa magonjwa ya zinaa au u mja mzito. Ni muhimu upewe dawa za kuzuia ugonjwa wa ukimwi kwa mda was masaa 72. Iwapo ulisumishwa ambia daktari achukue mkojo wako aupime.

Tafuta mahali pa faragha, mbali na aliyekudhulumu au aliyekushambulia. Muombe rafiki mwaminifu au jamaa akusaidie kwa kukuunga mkono hata akupatie mahali pa kuishi.

Kumbuka kuwa haupaswi kulaumiwa kwa yaliyokupata. Kupona kisaikologia na kimwili huhitaji muda. Nasaha bora itakufaa zaidi.


Watu waliodhulumiwa huonyesha dalili gani?

• Kuchanganyikiwa
• Kushindwa kulala vizuri
• Kuumwa na kichwa
• Uoga ama wasiwasi
• Kuchukilia kwa uzito zaidi jambo hata likiwa jepesi
• Majonzi na huzuni kuu
• Hasira
• Ndoto mbaya ama kukumbuka yaliyopita
• Kushindwa kabisa kuona roho au hata hisia za kimapenzi
Dhuluma za kinyumbani
Hizi ni dhuluma zinazoendelezwa na mme mtu au mke mtu wa kitambo, mpenzi wa kike au kiume na mtu mnayeishi naye. Mara nyingi wanawake na watoto ndio wanaotendewa dhuluma hizi. Hata hivyo pia wanaume wanaweza kutendewa dhuluma hizi.

Wanaodhulumu ni pamoja na mpenzi miliyetalikwana naye, wazazi wako, mlezi wako, mtoto wako au mtu yeyote ambaye mumewahi kuishi naye. (Hata kama mliyejumuika pamoja kwenye tafrija, mkajamiiana ama mmepata naye mtoto).

Dhuluma hizi hudhuru maisha ya anayedhulumiwa na watoto wake. Huweza kuishia kwa mtu kupelekwa hospitalini kutibiwa, kufungwa jela maisha, ama hata kusababisha kifo. Watoto ambao wamekua wakiona dhuluma hizi na watu ambao wamedhulumiwa wakiwa wazima, hata nao watawadhulumu wengine. Wanawake wanaovumilia dhuluma kwa muda mrefu mara nyingi huuawa na wapenzi (waume) wao kwa hivyo ni muhimu wapate usaidizi na wajiondoe katika mazingira haya.

Kuna msaada wakukusaidia kukabiliana na uhusiano wa kidhuluma unaotolewa bure.












Mbu waonyesha usugu vyandarua vyenye dawa




Mbu anayeambukiza malaria

Kuna taarifa kuwa mbu wameanza sugu haraka kwa vyandarua vilivyotiwa dawa, utafiti uliofanyika nchini Senegal umeonyesha.

Katika miaka ya karibuni matumizi ya vyandarua vyenye dawa yamekuwa ndio njia kuu ya kuzuia malaria hasa barani Afrika.

Kwa mujibu wa Jarida la Utafiti wa Kisayansi kwa magonjwa ya kuambukiza la Lancet, watafiti hao pia wanasema vyandarua hivyo vinapunguza uwezo wa kuhimili maradhi ya malaria kwa watoto wakubwa na watu wazima.

Lakini waatalam wengine wanasema utafiti huo ulikuwa mdogo kufikia maamuzi kuhusu uwezo wa vyandarua kwa muda mrefu.

Katika vita dhidi ya malaria silaha rahisi na yenye uwezo mkubwa moaka sasa imekuwa vyandarua vilivyotiwa dawa yamuda mrefu.

Katika miaka michache iliyopita vyandarua vimekuwa vikisambazwa barani Afrika na kwingineko –na Shirika la Afya Duniani –WHO linasema kama vikitumika vizuri vinaweza kupunguza nusu ya athari zinazotokana na malaria.

Iwapo huu ndio mwenendo tunaoushuhudia katika sehemu za Senegal basi ina umuhimu kwa siku zijazo katika mikakati ya kudhibiti na kuzuia malaria. Alisema Dr. Joseph Keating wa Chuo kikuu cha Tulane

Nchini Senegal, vyandarua vyenye dawa milioni sita vimesambazwa katika miaka mitano iliyopita. Katika utafiti huo uliofanyika katika kijiji kidogo nchini humo na kufuatilia matukio ya malaria kabla na baada ya kuanza kusambazwa kwa vyandarua hivyo mwaka 2008.

Katika kipindi cha wiki tatu tangu kuanza kutumika, wanasayansi walikuta kuwa maambukizi yalianza kushuka –matukio ya ugonjwa huo yalikuwa chini ya mara 13 kabla vyandarua havijaanza kutumiwa.

Watafiti pia walichukua sampuli za Anopheles gambiae, mbu mwenye kusambaza vilemelea vya malaria kwa watu Afrika. Kati ya mwaka 2007 na 2010 uwiano wa vijidudu vilivyokuwa sugu kwa aina moja ya dawa vilipanda kutoka 8% hadi 48%.









Viongozi wa Kiislamu waijadili Somalia





Viongozi na maafisa kutoka nchi 57 wanachama wa jumuia ya nchi za Kiislamu, wamekutana mjini Istanbul kuzungumzia njaa nchini Somalia. Mkutano huo umeitishwa na serikali ya Uturuki.

Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan pamoja na mkewe wanakusudia kuzuru Somalia baadae wiki hii ili kuitanabahisha dunia juu ya hali halisi wanayokabiliana watu wa Somalia.

Kwa serikali ya Uturuki kutumia muda wake mwingi kwa maswala ya Somalia ni ushahidi wa azma ya nchi hiyo ya kutanua ushawishi wake barani Afrika na katika nchi za Kiislamu licha ya kukabiliwa na migogoro kadhaa kwingineko kama vile mzozo katika nchi jirani ya Syria na machafuko katika eneo la wakurdi la kusini Mashariki .

Lakini wananchi wa Uturuki wameitikia vilivyo wito wa kusaidia wanaokabiliwa na maafa nchini Somalia kwa kutoa zaidi ya dola millioni mia moja za kimarekani.

Waziri mkuu Recep Tayyip Erdogan ameahidi kwenda Somalia baadae wiki hii pamoja na waziri wa mambo ya nje na wake zao.

Ziara za viongozi wa serikali ni nadra sana nchini Somalia.

Mkutano huu wa nchi za kiislamu uliitishwa na Uturuki li kuhimiza nchi ziongeze misaada yao na kuonyesha uungaji mkono kwa nchi za kiislamu wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Pia unasadifiana na malengo ya Uturuki barani Afrika ambako imeongeza idadi ya balozi zake katika miaka mitatu iliyopita na pia biashara yake kuongezeka kwa zaidi ya dola billioni saba kila mwaka.





Waziri mkuu wa Uturuki ziarani Somalia




Waziri mkuu wa uturuki Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kuwasili nchini Somalia kuanzisha rasmi kampeni ya kukabiliana na baa la njaa nchini humo.
Rais Sharif na BwErdogan

Raia wa uturuki wamechangia dola milioni 150 kusaidia somalia

Waziri huyo mkuu ataandamana na waziri wake wa mashauri ya nchi za kigeni na wake zao. Viongozi hao wamesema wako nchini Somalia kuonyesha wanawaunga mkono raia wa Somalia.

Raia wa Uturuki wamechanga kiasi cha dola milioni 150 hadi kufikia sasa kuisaidia Somalia.

Bendera za uturuki zimekuwa zikipaa katika uwanja wa ndege na bandari kuu mjini Mogadishu ikiwa ni ishara kuwa mji huo upo tayari kumpokea waziri mkuu Erdogan.

Ziara yake hii huenda ikawa na malengo mawili.

Moja ni kushuhudia harakati za kusamabaza misaada iliochangwa na raia wa nchi yake.

Pia kiongozi huyo na msafara wake wa mawaziri na wake zao pia unahamu kujionea wenyewe matatizo yanayo wakabili raia wa somalia.

Kando na misaada ya vyakula na madawa, raia wa uturuki wamechanga kiasi cha dola 115 milioni kusaidia walioathirika na njaa nchini humo.

Serikali ya uturuki pia inalenga sana kuongeza ushawishi wake barani Afrika.

Kando na mchango wake kibiashara, utawala huo unathamini bara hili ambalo kwa kiasi kikubwa kura zake zilisaidia nchi hii kupata nafasi ilionayo kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa.

Ikiwa waziri mkuu Erdogan atafaulu kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye mikakati ya kutatua mzozo unaoendelea nchini Somalia basi hii itakuwa njia moja ya nchi yake kupewa heshima barani humu na kwenye ngazi za kimataifa.




Mutharika afuta kazi mawaziri




Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika, amelifuta kazi baraza lake lote la mawaziri baada ya majuma kadha ya maandamano ya ghasia, ambapo watu karibu 20 wamekufa.
Maandamano ya Malawi

Bwana Mutharika sasa ameshika wizara zote 42; na hakutoa sababu ya kufanya hivo.

Mataifa kadha ya magharibi, yamesimamisha msaada kwa Malawi baada ya waandamanaji kuuwawa mwezi uliopita, ambao wakilalamika juu ya kupanda kwa gharama za maisha na kama walivosema, serikali mbovu.










Wapiganaji wa Libya wanajizatiti Zawiya



Wapiganaji wa Libya wanaendelea kusonga mbele kuelekea mji mkuu, Tripoli.
Wapiganaji wa Libya, mjini Zawiya

Televisheni ya wapiganaji hao imewaambia watu wajitayarishe kuwapokea.

Baada ya kuteka eneo la kati ya mji wa Zawiya, magharibi ya Tripoli, wapiganaji sasa wanasema wameiteka bandari muhimu ya Brega, mashariki mwa nchi, yenye kinu cha kusafisha mafuta.

Hakuna taarifa ya kuthibitisha hayo yanayotokea Brega.

Mwandishi wa BBC mjini Zawiya anasema kwenye medani wanayoiita medani ya mashujaa, katikati ya Zawiya, aliona majengo yaliyopigwa mabomu, yanayowaka moto, na kuta zenye matobo ya risasi.

Jana eneo hilo lilidhibitiwa kabisa na jeshi la Kanali Gaddafi.

Kulikuwa na mapigano makali jana jioni hadi usiku.

Lakini wapiganaji sasa wanaudhibiti mtaa, wamewatimua wanajeshi wa Gaddafi ambao wameelekea barabara ya kwenda Tripoli.

Kati ya medani alikuta maiti kama watatu.

Ameona maiti wanaoonesha kama Waafrika, na wapiganaji wanadai kuwa wanajeshi wengi wa Gaddafi ni askari mamluki kutoka kusini ya Sahara.

Ukweli hasa haujulikani, lakini maiti nyingi huko zinaonekana ni za Waafrika.

Sasa wapiganaji wanajitayarisha kusonga mashariki zaidi mwa mji, kuwatimua wanajeshi wa Gaddafi waliobaki Zawiya, ili kufungua njia ya kuelekea Tripoli.

Wapiganaji wa Libya wanadai kuwa waziri mkuu wa zamani, Abdessalem Jalloud, amekimbia Tripioli na amejificha katika maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji.







Misri itaondoa balozi wake Israil



Misri inasema kuwa imeamua kumuondosha balozi wake nchini Israel kwa sababu ya kuuwawa kwa askari wake wa usalama.
Wapalestina wanaangalia uharibifu kutokana na shambulio al Israil Gaza

Askari hao watano waliuwawa wakati wanajeshi wa Israil walipowaandama wapiganaji wa Palestina, ambao waliishambulia Israil Alkhamisi.

Huku nyuma Wamisri wameandamana mbele ya ubalozi wa Israil na kuchoma moto bendera ya Israil.

Misri imeilaumu Israil na imetaka kufanywe uchunguzi.

Israil imesema wanajeshi wake hawakuwa na makosa na kwamba itachunguza tukio hilo.

Taarifa ya serikali ya Misri inasema balozi wa Misri ataondoshwa hadi Israil itapochunguza vifo vya askari watano wa usalama wa Misri.

Jeshi la Israel limeahidi kufanya uchunguzi.

Misri imesema yaliyotokea ni kinyume na mkataba wa amani baina ya Israil na Misri.

Balozi wa Israil mjini Cairo ameitwa Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje kwa majadiliano zaidi.

Huku nyuma, waandamanaji nje ya ubalozi wa Israil mjini Cairo, wameipuuza taarifa iliyotolewa, na walipiga kelele na kuchoma moto bendera ya Israil.

Baadhi ya waandamanaji walibeba picha ya Hayati Rais Gamal Abdel Nasser, ambaye akijulikana kuwa dhidi ya Israil, na akitaka umoja wa nchi za Kiarabu.

Tangu mashambulio ya Alkhamisi, ndege za Israil zimeshambulia eneo la Gaza mara kadha, huku wapiganaji wa Kipalestina wameirushia Israil makombora zaidi ya 20.







Mapambano ya kikabila Sudan Kusini




Wakuu wa Sudan Kusini wanasema watu zaidi ya 500 wameuwawa kwenye mapigano ya kikabila katika jimbo la Jonglei, mashariki mwa nchi.
Bendera ya Sudna Kusini ikipandishwa

Afisa wa eneo hilo (Gabriel Duot Lam) ameiambia BBC kwamba watu mia kadha wamejeruhiwa na zaidi ya 200, wengi wakiwa watoto, walitekwa nyara.

Mapigano hayo yalitokea Alkhamisi, wakati watu wa kabila la Murle inasemekana waliwashambulia Lou Nuer,


na kuwaibia ng'ombe kama elfu 40.

Sudan Kusini ilipata uhuru mwezi uliopita na inakabili matatizo makubwa kuhusu usalama.








Tanzania yapiga marufuku uuzaji wanyama





Twiga


Tanzania imetangaza kuwa inapiga marufuku biashara ya kukamata na kuwasafirisha wanyamapori kwenda nje ya nchi.

Hatua hiyo imetangazwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akijibu hoja bungeni kuhusu madai kwamba wanyama takriban 130 wakiwemo ndege 16 walitoroshwa kinyume cha sheria mwishoni mwa mwaka jana na kusafirishwa kwenda nchi moja ya Mashariki ya Kati.

Katika jibu lake Bw Pinda alisema: “Kwanza tunataka tukubaliane na mawazo ya wabunge kwa ujumla kwamba, inaonekana eneo hili bado utaratibu wake wa usimamizi na hata namna biashara yenyewe inavyofanyika, ni eneo ambalo kwa kweli linahitaji kutazamwa upya.

“Kwa hiyo, kama serikali tumeamua kwamba, tutasimamisha usafirishaji au biashara za wanyama zote na tuangalie tena upya jambo hili na ikitokea kwamba tunakubaliana tuendelee nalo, ni dhahiri na lazima masharti yabadilike.”

Wabunge wa chama tawala pamoja na upinzani wamekuwa wakiishutumu serikali kwa kuifumbia macho kashfa hiyo.

Lakini kwa uamuzi iliofanya, serikali imeonekana kujipunguzia shutuma na kupata kuungwa mkono na wabunge wa kambi zote mbili.
Shutuma

Hata hivyo hitimisho hilo halikufikiwa bila serikali kujeruhiwa vibaya na wabunge. Hoja hizo nzito zilianza kusikika tangu mwanzoni mwa mjadala wa makadirio ya bajeti ya wizara ya maliasili na utalii kwa mwaka 2011/2012.


Mbunge Christopher Ole-Sendeka wa jimbo la Simanjiro kupitia chama tawala cha CCM alisema tukio hilo limeidhalilisha serikali na vyombo vyake vya dola vyenye majukumu ya kusimamia usalama wa nchi.

“Kinachotia fedheha kuliko yote ni kwamba, waliofanya kazi hiyo walipewa zawadi nyingine ya kupandishwa vyeo. Nataka niseme wazi kuwa mkurugenzi wa wanyamapori wa sasa, ndugu Mbangwa, hawezi kukwepa lawama ya kutoroshwa wanyama hao,” alisema Ole Sendeka aliyeonekana kuungwa mkono na wenzake.
Hatua za serikali

Habari za kutoroshwa wanyama zilianza kusikika tangu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini mjadala wa bajeti ya Wizara ya maliasili na utalii ndiyo imeibua maswali mazito dhidi ya serikali ambayo imelazimika kutoa majibu na kuchukua hatua.

Waziri wa maliasili na utalii Ezekiel Maige aliposimama kujibu hoja zilizotolewa na wabunge wa pande zote mbili alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema serikali imekuwa ikilifanyia uchunguzi kwa muda wa miezi kadhaa.

Vile vile waziri huyo alitangaza kuwasimamisha kazi maafisa waandamizi wa Idara ya wanyamapori, akiwemo mkurugenzi mkuu Obeid Mbangwa, ili kuwezesha uchunguzi ufanyike kubaini swala hilo lilifanyika katika mazingira ya gani.

Tanzania inategemea utalii kwa asilimia takriban 17 ya mapato yake, ambapo kwa mwaka huu utalii unatarajiwa kuvuna dola bilioni 1.7. Wanyama ni sehemu muhimu ya vivutio vya Tanzania.






Shambulio ofisi ya Uingereza Afghanistan
Kabul




Shambulio Kabul


Washambuliaji waliojitoa mhanga wameshambulia afisi za British Council katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, na kuwaua takriban watu tisa na kushikilia eneo la afisi hizo kwa saa kadhaa.

Bomu liliotegwa ndani ya gari liliangamiza ukuta unaozingira ua na watu kadhaa waliokua wamebeba silaha nzito wakavamia sehemu za ndani.

Baada ya mapambano ya saa kadhaa Balozi wa Uingereza mjini Kabul alisema washambuliaji wote waliuwawa. .

Kundi la Taleban limesema shambulio hilo linaadhimisha uhuru wa Afghanistan kutoka Uingereza mnamo mwaka 1919.

Takriban askari polisi wanane wa Afghanistan na afisa mmoja wa usalama ambae inaarifiwa ni nimwanajeshi wa huduma maalum wa New zealand waliuwawa.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alilaani mashambulio hayo "ya kioga" akisema ameongea na Waziri Mkuu wa New Zealand John Key kumshukuru kwa mchango wa vikosi maalum vya nchi yake katika kulinda eneo hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya Uingereza imesema raia wote wa Afrika Kusini wamepigwa na mshtuko lakini wako salama baada ya kuhamishwa kutoka jengo hilo.

Balozi wa Uingereza William Patey amesema kuna majeruhi miongoni mwa wanajeshi wa zamani waNepali wa kikosi cha Gurkha-lakini hakuna aliyekufa.









ANC ya Afrika Kusini kumuadhibu Malema





Julius Malema, kiongozi wa Vijana wa ANC

Mkutano mkuu wa chama tawala cha ANC nchini South Africa umeamua kumuadhibu kiongozi wa vijana Julius Malema kwa kuchafua sifa ya chama hicho.

Tuhuma za hivi karibuni zinatokana na kauli zake kuwa Umoja wa Vijana wa ANC utafanya uwezalo kuanzisha mabadiliko ya utawala wa nchi jirani ya Botswana.

Bw Malema alikuwa ‘akipanda mbegu za mgawanyiko’ ndani ya chama, ANC imesema.

Ni kiongozi mashuhuri Afrika Kusini lakini maoni yake kuhusu kutaifisha madini na mashamba yamesababisha hisia tofauti kutoka kwa umma.

"Komredi Julius Malema amekuwa akituhumiwa kwa matukio kadhaa ya kuvunja katiba ya ANC ikiwemo kuiingiza ANC katika migogoro kupitia kauli na matamshi yake kuhusu Botswana na kupanda mbegu za mgawanyiko katika uongozi wa Chama," Chama hicho kilisema katika taarifa yake.

ANC kinasema suala lake sasa limo mikononi mwa Kamati ya Maadili ya ANC, ambayo itaamua tarehe, mahali na muda wa kusikiliza tuhuma hizo.

Mapema wiki hii, Bw Malema amekiomba radhi ANC kwa kusema kuwa utawala wa serikali ya Botswana ni wa vibaraka na ni tishio kwa Afrika.









Msaada wa Somalia utafika kwa walengwa





Bw Andrew Mitchell

Uingereza "haitovumilia" ufisadi unaozuia jitihada za kupambana na njaa Somalia, waziri mwandamizi mmoja alisema.

Andrew Mitchell alisema alizungumzia suala hilo na waziri mkuu wa Somalia alipotembelea nchi hiyo siku ya Jumatano.

Alisema umma wa Waingereza unaochangia fedha katika wiki za hivi karibuni unahakikishiwa msaada unawafikia wale wanaostahili na si kufikishwa kwa wasiokusudiwa.

Serikali hiyo imeahidi dola za kimarekani milioni 25 zaidi kwa ajili ya chakula na dawa kusaidia watu 400,000 ambao wako katika hatari ya kufariki dunia.

Bw Mitchell alikuwa akizungumza baada ya kurejea kutoka mji mkuu wa Somalia ulioathirika na vita- ziara ya kwanza iliyofanywa na waziri kutoka Uingereza kwa kipindi cha miaka 18.

Ameonya kuwa "wanakimbizana na muda" kutatua ukame uliokithiri nchini humo na bila hatua za haraka maelfu ya watoto wanaweza kufa kwa njaa.

No comments:

Post a Comment