KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, July 8, 2011
Saa chache kuelekea Uhuru Sudan Kusini
Wasudani Kusini katika sherehe za kuzaliwa Taifa jipya
Sudan Kusini inahesabu saa chache ili kuwa Taifa jipya kabisa kuzaliwa duniani Jumamosi ya Julai 9.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir na wageni wengine mashuhuri kutoka kote duniani watahudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika mji mkuu Juba.
Zaidi ya asilimia 99 ya Wasudan Kusini walipiga kura kujitenga na Sudan Kaskazini katika kura ya maoni iliyofanyika mwezi Januari.
Kura hizo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2005 kumaliza miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha watu 1.5 milioni kufa.
Nchi mpya ya Sudan itakuwa na utajiri wa mafuta lakini itakuwa moja ya nchi maskini kabisa duniani kutokana na mapigano ya muda mrefu.
Sherehe zitaanza baada ya saa sita usiku saa za Sudan (2100 GMT) kwa kuhesabu dakika chache kufikia saa kamili ya kuwanza kwa siku wakitumia saa kubwa katikati mwa Juba.
Mwandishi wa BBC Will Ross anasema katika kuelekea kwenye tukio hilo la kihistoria, vituo vya redio vimekuwa vikipiga wimbo mpya wa Taifa la Sudan Kusini.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir
Mapema wiki hii Bw Bashir aliahidi kuiunga mkono Sudan Kusini na kusema kuwa anataka Taifa hilo jipya kuwa ‘salama na lililotengamaa.
"Tutawabariki ndugu zetu wa Kusini nchini mwao na tunawatakia mafanikio" alisema Bw Bashir, aliyekubaliana na mkataba wa amani na chama cha Sudan People's Liberation Army (SPLA).
Lakini ameonya kuwa ‘Uhusiano wa kindugu’ utategemea na mipaka salama na kutoingilia masuala ya nchi jirani (Kusini au Kaskazini)
"Kwa hiyo tunafuraha sana na tunashukuru kwa mchango ao kwa Taifa hili."
Rebecca Garang, mke wa hayati John Garang
Kulikuwa na wasiwasi huenda vita vingezuka tena baada ya mapigano mapya ya hivi kribuni katika maeneo ya mpakani Abyei na Kordofan Kusini ambayo yalilazimisha watu 170,000 kukimbia makazi yao.
Hata hivyo makubaliano tofauti ya wiki za hivi karibuni na kuondoa vikosi kwenye mipaka kumerejesha hali ya utulivu.
Rebecca Garang, mke wa hayati John Garang aliyeongoza waasi wa Sudan katika vita vya wenyewe kwa wenyewe , ameiambia BBC kuwa watu wake hawana matatizo na watu wa Kaskazini isipokuwa serikali yao.
"Kuna rafiki zetu wengi tu ambao walikufa wakati w vita lakini tuko hapa kwa ajili ya damu yao," alisema.
Muhimu kuhusu Sudan Kusini
Idadi ya watu: 7.5-9.7 milioni
Ukubwa: 619,745 kilometa za mraba (239,285 maili), kubwa kuliko Uhispania na Ureno zikijumuishwa pamoja.
Lugha kuu: Kiingereza, Kiarabu (zote ni rasmil), Kiarabu cha Kijuba, Kidinka
Dini: Za kijadi/asili, Wakristo kidogo
Biashara ya nje: Mafuta
Moja ya nchi maskini kabisa duniani: Idadi kubwa ya vifo vya akina mama wajawazito; watoto chini ya miaka 13 hawasomi; 84% ya wanawake hawajui kusoma na kuandika.
Uhusiano na Sudan: Kugawana madeni na mafuta ; migogoro ya mipaka; uraia
Usalama: Takriban vikundi saba vya waasi
Changamoto za mbele
Wakati huohuo, Marekani imeitaka serikali ya Bw Bashir kuyaruhusu majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani kuendelea kubakia kaskazini, kufuatia vitisho kutoka Khartoum kuyafukuza kutoka majimbo ya Kaskazini ya Kordofan Kusini na Blue Nile.
"Ni muhimu kwa Umoja wa Mataifa kuruhusiwa kulinda amani kikamilifu katika maeneo hayo kwa kipindi kirefu zaidi," alisema Susan Rice, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa.
Mwandishi BBC anasema kuifanya Sudan ya Waislam Kaskazini na Kusini kuwa tulivu kwa muda mrefu baada ya sherehe kuisha itakuwa ni changamoto kubwa.
Pande zote mbili lazima zikamue juu mambo kama kuweka mpaka mpya na namna ya kugawana madeni na utajiri wa mafuta.
Wachambuzi wanasema kipaumbele kwa Khartoum kitakuwa kufanya mazungumzo juu ya mkataba mzuri wa mapato ya mafuta kwa sababu visima vingi viko Kusini.
Kwa sasa, mapato hayo yanagawanwa sawa kila upande.
Ajali ya ndege yatokea DRC
Ndege ya abiria iliyokuwa na watu 112 imeanguka kwenye uwanja wa ndege wa Kisangani huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Takriban watu 40 wamekutwa wakiwa hai, lakini wengine zaidi ya 50 wanasemekana kufariki dunia.
Kisangani
Ndege hiyo, iliyo chini ya shirika la ndege la Hewa Bora, ilijaribu kutua baada ya hali ya hewa kuwa mbaya ikitokea Kinshasa.
Hakuna uthibitisho bado wa aina ya ndege iliyohusishwa.
Mkurugenzi mkuu wa Hewa Bora Stavros Papaioannou aliliambia shirika la habari la Reuters, " Rubani alijaribu kutua lakini hakufanikiwa kugusa barabara ya ndege."
Msemaji wa serikali Lambert Mende alisema ndege hiyo iligonga karibu sana na uwanja wa ndege huku kukiwa na radi.
Alisema, " Tumejitahidi kuwaokoa watu 40 na harakati za uokoaji zinaendelea".
'Mbakaji' wa Congo Kanali 'Kifaru' Kulimushi ajisalimisha
Huku shughuli za uokoaji zikiendelea mwanajeshi mwenye cheo cha Kanali anayeshutumiwa kwa ubakaji wa watu wengi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amejisalimisha kwa jeshi hilo.
Msemaji wa jeshi alisema Kanali Nyiragire "Kifaru" Kulimushi amejisalimisha pamoja na zaidi ya wapiganaji wake 150, wanaoshutumiwa pia kwa ubakaji wa wanawake wengi.
Wanawake walioathiriwa na ubakaji
Mwezi uliopita, takriban wanawake 100 waliwashutumu waliokuwa waasi waliojiunga na jeshi la nchi hiyo kwa kuwadhalilisha kijinsia katika jimbo la Kivu ya Kusini.
Ujumbe wa umoja wa mataifa mwaka jana umeelezea nchi hiyo ya Congo kama "mji mkuu wa ubakaji duniani".
Ghasia zilizodumu miaka 16 mashariki mwa Congo zimesababisha kuenea kwa udhalilishaji wa wanawake na watoto wa kike.
Msemaji wa jeshi Lt Kanali Vianney Kazarama ameiambia BBC kuwa Kanali Kifaru alijisalimisha baada ya kutoka misituni kwenye ngome yake iliyopo mashariki mwa Congo.
Alisema, "walikuwa 150, na silaha zao-zikiwemo silaha nzito".
Wafadhili waguswa na athari za ukame
Serikali ya uingereza tayari imetoa dola milioni 61 kusaidia walioathirika
Mashirika ya kutoa misaada nchini Uingereza yameanzisha harakati za kuchangisha pesa kusaidia watu wanaokabiliwa na njaa Afrika Mashariki.
Mashirika hayo yamelenga kusaidia watu milioni 10 ambao wameathrika zaidi na ukame nchini Somalia, Kenya, Ethiopia na Sudan Kusini.
Tayari serikali ya Uingereza imeahidi kutoa dola milioni 61 kusaidia harakati hizo za kutoa misaada wa vyakula na huduma za matibabu katika eneo hilo.
Pesa hizo zitasaidia kutoa misaada ya dharura kwa watu milioni 1.3
Kulingana na Umoja wa Mataifa hii ndio hali mbaya zaidi ya ukame kushuhudiwa katika upembe wa Afrika kwa kipindi cha miaka 60.
Inakisiwa kuwa watu 1,300 wanahama makaazi yao nchini Somalia kila siku kuingia Kenya na Ethiopia kwa sababu ya athari za ukame.
Mashirika hayo yamebuni kamati maalumu ya kushughulikia janga hilo na yanaungwa mkono na BBC katika juhudi zao za kuchangisha pesa hizo.
Maelfu ya watu hasaa raia wa Somalia wanahitaji misaada hiyo na wengi wamepewa hifadhi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab ilioko kaskazini mashariki mwa Kenya.
Rais wa Yemen atokea kwenye televisheni
Rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh sasa
Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen amelihutubia taifa lake kwa njia ya televisheni kwa mara ya kwanza tangu kuungua katika shambulio liliofanywa katika kasri yake mwezi uliopita.
Bw Saleh amekuwa akifanyiwa matibabu nchini Saudi Arabia tangu tarehe 6 Juni baada ya shambulio ambalo wakuu wa serikali ya nchi hiyo walisema yalisababishwa na bomu.
Akiongea kutoka Saudi Arabia Rais Saleh amesema amefanyiwa operesheni nane kutibu majeraha ya kuungua na kwamba zote zimefanikiwa.
Rais Ali Abdullah Saleh wa Yemen
Mikono yake ilikuwa imefungwa bandeji na alisisitiza haja ya mazungumzo ili kuyatanzua matatizo ya Yemen.
Kwa muda wa miezi kadhaa sasa Yemen imekumbwa na machafuko, huku waandamanaji wakidai Bw Saleh ajiuzulu.
Lakini amekataa kujiuzulu na amezipuuza juhudi zote za kuleta upatanishi kati yake na waandamanaji.
Yemeni President Ali Abdullah Saleh, his face burned and his hands covered with bandages, has appeared on television for the first time since he was wounded in a bomb attack on his palace in Sanaa, Al Jazeera reported.
Saleh, who was hospitalised in Saudi Arabia after the June 3 attack, said he had undergone "more than eight successful operations" and called for dialogue in his speech broadcast on Yemeni television on Thursday.
In his brief address, recorded in Saudi Arabia, he said those who have sought to drive him from power had an "incorrect understanding of democracy".
More than four months of popular uprising seeking to push the longtime ruler from power have shaken the impoverished Arabian peninsula country.
Saleh said he welcomed power sharing as long as it was within the country's constitutional framework.
State television showed fireworks lighting up the sky above the capital at the end of Saleh's speech, as the president's supporters celebrated his appearance.
"Where are the men who fear God? Why don't they stand with dialogue and with reaching satisfactory solutions?" Saleh asked during his speech.
He also thanked Abdrabbu Mansour Hadi, the vice president, who has come under domestic and international pressure to assume power during the president's absence, "for his efforts in bridging gaps between all political parties".
Ameen Al Himyari, a Qatar University professor, told Al Jazeera that the US is not placing enough pressure on Saleh to step down.
"The interest of the Americans and the Saudis is to support the protestsers, the revolution. It's peaceful and they can guarantee security," Al Himyari said.
"Supporting the corrupt regime its going to create a lot of problems."
'Disappointment'
Al Jazeera's Sherine Tadros, who has reported extensively from Yemen, said: "I think it will come as a disappointment to tens of thousands of people who have been protesting in Sanaa.
"They were watching this message to try to figure out if he is going to come back and if there is going to be some kind of transition of power.
"But the main thing here is that we saw him in vision. We've been waiting for this message for weeks. Since the explosion we were told that he was going back to Yemen.
"Certainly when people watched him, they would see a man who looks defeated in some way, without his glasses and suit. He didn't look his normal self. He was in his tone defiant and in his speech very eloquent.
"There is a feeling there that the vice president is a more conciliatory figure in the country. When I was in Yemen at the beginning of the protests, the meetings with the opposition would take place at the VP's house.
"The VP is a good figure to take this forward. But the reality on ground is that most of the power - when it comes to security - is still in hands of [Saleh's] sons and nephews."
Syria yaishtumu Marekani
Syria imeishtumu Marekani kwa "kuingilia" masuala yao ya ndani baada ya balozi wa Marekani nchini humo kusafiri hadi katika eneo la machafuko la mji wa Hama.
Wizara ya mambo ya nje ya Syria inasema ziara hiyo ya Robert Ford ilikuwa "ushahidi wazi" kuwa Marekani inahusika na maandamano yanayoendelea nchini humo.
Mapema, Wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema kuwa ziara ya Bwana Ford ilikuwa ni kuwaunga mkono waandamanaji.
Mamia ya wakaazi wa Hama wamekimbia wakiogopa kushambuliwa na vikosi vya usalama.
Balozi wa Marekani nchini Syria Robert Ford
Vifaru vya kijeshi vimewekwa nje ya mji na takriban watu 22 wameuawa katika siku za hivi karibuni.
Serikali ya Marekani inasema kuwa Bwana Ford anatarajiwa kubaki Hama kwa ajili ya maandamano dhidi ya serikali ambayo kwa kawaida hufanyika baada ya sala ya Ijumaa.
Mwandishi wa BBC Kim Ghattas mjini Washington amesema kuwepo kwa balozi wa Marekani mjini Hama kunaweza kumkamfanya Rais wa Syria Bashar al-Assad kushindwa kufanya mashambulio makali eneo hilo.
Lakini hatua hiyo imekera sana serikali ya Syria.
Maandamano
" Kuwepo kwa balozi wa Marekani mjini Hama bila ruhusa ni dhihirisho wazi la matukio ya hivo karibuni,na jaribio lao la kutaka kuzidisha machafuko, ambayo yanaharibu usalama na amani ya Syria," wizara ya mambo ya nje ilisema katika taarifa.
Maandamano ya Ijumaa iliopita mjini Hama yalikuwa moja ya maandamano makubwa katika muda wa miezi mitatu kuwahi kufanyika nchini Syria.
Siku moja baadaye, Bwana Assad alimfuta kazi gavana wa eneo hilo Ahmad Khaled Abdel Aziz kwa kushindwa kukabiliana na maandamano hayo.
Biashara zafungwa Uganda siku ya pili
Wafanya biashara katika mji mkuu wa Uganda, Kampala wamefunga maduka yao kwa siku ya pili mfululizo kulalamikia kiwango cha sarafu ya nchi hiyo kinachoshuka kila kukicha pamoja na idadi kubwa ya wachuuzi wenye asili ya Kichina.
Uganda
Shilingi dhaifu kwa Dola
Wauza maduka wanadai kuwa sarafu dhaifu inapandisha bei za bidhaa kutoka nje.
Wakati huo huo wanasema hawawezi kushindana na wafanya biashara wa Kichina waliomimina bidhaa zao kwa wingi na kwa bei rahisi.
Mgomo wao wa siku mbili ni tukio la hivi sasa katika mfululizo wa maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha nchini Uganda.
Polisi wa kuzuia fujo walikuwa mitaani kulinda doria katika mji wa Kampala, kuzuia uwezekano wa kuzuka ghasia.
Polisi wanalinda doria Kampala
Msemaji wa shirika la wafanyabiashara la jiji la Kampala, Issa Sekito amesema kua wamefunga maduka yao kuishinikiza serikali ishughulikie masaibu yao.
Bw.Sekito amesema kua shirika lake limeitaka serikali ushughikie biashara za Wachina ambao wamezidsha kujiimarisha nchini Uganda.
Bw.Sekito aliliambia gazeti moja la nchini Uganda kuwa ''Kwa mda sasa,tumekua tukiilalamikia serikali juu ya hawa wageni wanaoshiriki biashara ndogo ndogo,hususan Wachina, wanaokuja wakidai eti ni wawekezaji''
Shilingi ya Uganda ilidondoka kufikia kiwango cha chini dhidi ya dola ya Marekani mwezi uliopita hadi Benki kuu ilipoingilia kati kujaribu kuiimarisha.
Shirika la habari la Reuters limearifu kuwa 'Mgomo huo umesababisha bei ya bidhaa kama sukari na chumvi kupanda nchini humo''.
Mkaazi mmoja wa mji wa Kampala aliyehojiwa na shirika hilo, Linda Sempijja alisema kuwa maisha yamekuwa magumu kwa sababu bei ya bidhaa zote imepanda.
Mkaazi huyo aliongezea kusema kuwa hawezi kuwalaumu wafanyabiashara, kwa sababu wao pia wanakabiliwa na hali ngumu. Nailaumu serikali, alisema.
Gazeti la kiserikali la New Vision limearifu kuwa Waziri wa Biashara na viwanda,Bi.Amelia Kyambadde alikutana na wafanyabiashara kwa mda wa saa sita.
Waziri huyo aliwasilisha ujumbe kutoka kwa Rais Museveni akiwahimiza wasimamishe mgomo wao, kwa mujibu wa gazeti hilo.
Wafanyabiashara, hata hivyo walisema hawatofungua maduka yao na kwamba mgomo wao utaendelea hata siku ya leo alhamisi.
Wadadisi wanasema kuwa mgomo wao ni ishara ya hivi karibuni inayoonyesha hali ya ongezeko la kutoridhia kwa wananchi kwa serikali ya nchi.
Mnamo mwezi Aprili, vyama vya upinzani vilianzisha maandamano ya kususia usafiri wa umma na kutembea kwenda kazini, kama ishara ya kuitaka serikali itambue ukweli wa kupanda kwa gharama za maisha.
Ghasia zilianza Febuari
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa vikosi vya usalama viliua watu tisa walioshiriki maandamanao hayo.
Serikali ilivilaumu vikundi vya upinzani kwa kujaribu kuteka madaraka kupitia ghasia baada ya kushindwa katika Uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi Febuari.
Polisi yazima maandamano kwa gesi kali
Polisi nchini Kenya imetumia gesi ya kutoza machozi kutawanya mamiya ya waandamanaji mjini Nairobi wakipinga kupanda kwa bei ya chakula na mafuta.
Polisi wazima maandamano
Mwandishi wetu, Robert Kiptoo akiwa mjini Nairobi anasema kuwa ummati huo wa watu ulipita katikati ya jiji ukiimba nyimbo za kukashifu wakati wakizuia mtiririko wa magari na kusababisha wenye maduka kuyafunga.
Kuna uhaba wa mahindi kote Afrika mashariki kutokana na ukame.
Serikali ya Kenya hivi karibuni ilipunguza kodi juu ya mahindi yanayoagizwa kutoka nje ili kuepusha kupanda kwa bei.
Maandamano kupinga gharama kubwa
Wanafunzi kadhaa wa Chuo kikuu na wanaharakati za haki za utu walikamatwa wakati wa maandamano ambayo Polisi waliyataja kama yaliyofanywa bila kufuata utaratibu wa sheria sababu hawakuomba ruhusa kuandaa maandama
Baadhi ya waandamanaji walisoma vipengee katika Katiba mpya , vilivyoongezewa mwaka jana, wakielezea haki yao ya uhuru wa kuandamana, anasema mwandishi wetu.
Hata hivyo juhudi zao za kufika kwenye afisi ya Rais na Waziri mkuu kuwasilisha malalamiko yao zilikwama pale Polisi wa kuzia fujo walipotumia gesi ya kutoza machjozi na mbwa kuwatawanya.
Mwandishi wetu anasema kuwa kupanda kwa gharama za maisha kumewaudhi raia wengi wa Kenya.
Bei ya hii leo ya mfuko wa kilo mbili ya unga wa mahindi ni sawa na dola mbili za Marekani au pauni 1.25 za Uingereza.
Bei hiyo ni kubwa kwa raia milioni 40 wa Kenya.
Waandamanaji hao pia wamewatuhumu wenye viwanda vya kusaga mahindi kwa kuhodhi mahindi ili kuona kuwa bei inapanda.
Watu takriban milioni 12 katika pembe ya Afrika wamekumbwa na ukame - ambao haujatokea katika eneo hili katika kipindi cha miaka 60.
Halikadhalika Kenya inakabiliana na mfumko wa bei huku sarafu yake ikiwa imeshuka kiasi ikilinganishwa na dola ya Marekani.
Gazeti la 'udaku' Uingereza kufungwa
Gazeti kufungwa
Gazeti la kila Jumapili la News of the World la Uingereza lilatoka kwa mara ya mwisho siku ya Jumapili, siku chache baada ya tuhuma nzito kuliandama gazeti hilo.
Mwenyekiti wa kampuni inayomiliki gazeti hilo la News International, James Murdock amesema toleo la Jumapili ndio litakuwa la mwisho.
Gazeti hilo la kila wiki linatuhumiwa kufanya udukuzi wa simu kwa waathirika wa uhalifu, watu mashuhuri na wanasiasa.
Siku ya Alhamisi, polisi wa Uingereza walisema watawatafuta watu wapatao 4,000 ambao wametajwa kufanyiwa udukuzi katika nyaraka ambazo zimepatikana.
Gazeti hilo ambalo linasomwa zaidi nchini Uingereza limekuwa likitoka kwa miaka 168.
News of the World ambalo huuza nakala takriban milioni 2.8 kila wiki, limepata umaarufu kwa kutoa habari motomoto za watu maarufu na kufichua kashfa mbalimbali.
Ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza imesema haihusiki kwa njia yoyote katika uamuzi wa kulifunga gazeti hilo.
Bw Murdoch amesema hakuna matangazo yoyote yatarushwa katika gazeti hilo wiki hii, badala yake nafasi za matangazo zitatolewa kama sadaka, na hata mapato ya gazeti hilo yatatolewa kama msaada.
Kampuni ya News International imegoma kusema lolote kuhusiana na uvumu kuwa huenda gazeti lake la Sun sasa litatoka kila siku hadi Jumapili.
Waasi wasonga mbele kukaribia Tripoli
Waasi wa Libya wako kilometa 100 kusini magharibi mwa Tripoli
Waasi wa Libya wanasema wamesonga mbele katika kijiji cha Gualish
kilometre 100 (maili 60) kusini magharibi mwa mji mkuu Tripoli.
Mapumziko kwenye makazi madogo jangwani ni muhimu kuelekea katika ngome kubwa mjini Garyan ambayo inadhibiti barabara kuu inayoelekea mji mkuu Tripoli.
Waasi hao walisema wamedhibiti maeneo kadhaa ya wanajeshi wa serikali.
Kwa upande wa magharibi mwa nchi vikosi vya waasi vimesonga mbele kuzunguka mji wenye bandari wa Misrata.
Taarifa zinasema waasi wanaopigana na Kanali Muammar Gaddafi walivamia Gualish siku ya Jumatano baada ya mapigano yaliyoudumu kwa saa kadhaa.
Taarifa nyingine zinasema waasi wamedhibiti maeneo muhimu ya makazi magharibi ambako kuna kituo cha Umeme na mnara wa maji.
Takriban waasi wanne wameuawa na 17 kujeruhiwa, daktari mmoja wa karibu na Yefren alisema.
Simba yatinga fainali
Simba ya Tanzania
Klabu ya soka ya Simba ya Tanzania imeingia fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati, Kagame Cup baada ya kuisambaratisha timu ya Al Mereikh ya Sudan kwa njia ya mikwaju ya penati 5 -4.
Mikwaju ya penati ilifuatia baada ya dakika 90 na hatimaye dakika 30 za nyongeza kutozaa matunda katika mechi ya kukata na shoka iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
Huenda sifa na pongezi zikamiminika kwa mlinda mlango wa Simba Juma Kaseja ambaye ndiye aliyewapeleka fainali baada ya kuokoa penati ya mwisho iliyopigwa na Al Mereikh.
Timu hizo zilingia katika hatua ya kupigiana penati baada ya kumaliza dakika 120 zikiwa zimefungana 1 - 1.
Simba sasa itacheza fainali siku ya jumapili na mshindi wa mechi kati ya Yanga ya Tanzania na St. George ya Ethiopia ambaye atajulikana siku ya Ijumaa.
Yanga na St. George zitamenyana siku ya Ijumaa katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano hiyo.
Kwa matokeo hayo Al Mereikh sasa itacheza mapema siku ya jumapili kutafuta nafasi ya mshindi wa tatu ya michuano hiyo ya CECAFA na timu itakayoshindwa kuingia fainali kati ya Yanga ya Tanzania na St. George ya Ethiopia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment