Waandamanji nchini Libya
Wagombea haki za kibinaadamu wanasema watu kama 84, wameuawa katika maandamano nchini Libya.
Mwandishi wa BBC, katika Mashariki ya Kati anasema hata hivyo, idadi hiyo iliyotolewa na shirika la Human Rights Watch, inaweza kuwa ni ndogo.
Fujo nyingi zimetokea katika mji wa Benghazi ambako inaelekea wapinzani wa serikali wanadhibiti mitaa kadhaa.
Inaarifiwa kuwa kikosi maalumu cha jeshi, sasa kimewasili mjini humo.
Pia kuna mapambano katika miji kama mitano mengine.
Ghasia kidogo pia zimetokea katika mji mkuu, Tripoli, shina la madaraka ya Kanali Ghadaffi
No comments:
Post a Comment