KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, February 19, 2011
Wanawake watano wauawa Ivory Coast
Majeshi ya usalama nchini Ivory Coast yamewapiga risasi wanawake watano waliokuwa wakiandamana kumwunga mkono Alassane Ouattara kwenye mji mkuu wa Abidjan, walioshuhudia wamesema.
Wafuasi wa Alassane Ouattara
Bw Ouattara anatambuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba, lakini Bw Gbagbo amekataa kuachia madaraka.
Wanawake hao walifyatuliwa risasi wakiwa Abobo, eneo linalomuunga mkono Ouattara.
Idrissan Diarrassouba mkaazi wa Abobo aliliambia shirika la habari la Reuters watu waliokuwa wamevaa sare za jeshi walianza kuwafyatulia risasi wanawake hao kiholela.
Wanawake hao walikuwa wanachama wa shirika la kisiasa la RHDP.
Mwandishi wa BBC, John James, alisema shughuli nyingi za nchi hiyo zimesimama baada uchaguzi uliofanyika miezi mitatu iliyopita.
Vikwazo wa kimataifa vinavyokusudiwa kumshurutisha rais Gbagbo kuachia madaraka vimesababisha biashara kupungua nchini humo huku magenge ya vijana yameweka vizuizi barabarani katika miji mikuu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment