KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, February 16, 2011

Ruksa Wanaume Kuwaoa Wanaume Wenzao Kanisani


Serikali ya nchini Uingereza inapitisha sheria wiki hii ambayo itabadili maana halisi ya ndoa na kufanunua kuwa ndoa si lazima iwe ni mwanamke na mwanaume bali watu wa jinsia moja nao wanaweza kuoana na pia ndoa zao kufungwa kanisani.
Watu wa jinsia moja wataweza kufunga ndoa kanisani kwa mujibu wa sheria mpya zinazotarajiwa kutangazwa wiki hii nchini Uingereza.

Mashoga na wasagaji wataweza kufunga ndoa kanisani na sherehe zao zitaongozwa na wachungaji na viongozi wengine wa dini.

Mbali ya ruhusa hiyo, serikali ya Uingereza ina mpango wa kuibadili maana ya ndoa katika katiba ambapo ndoa ilikuwa ikijulikana kuwa ni kati ya watu wa jinsia mbili tofauti, mwanamke na mwanaume.

Sheria hiyo mpya itawawezesha wanaume kuwaita wanaume wenzao "Mume wangu" au "Mke wangu" hali kadhalika kwa wanawake nao wataweza kuitana mume na mke.

Kanisa la Anglikana limesema kuwa litakubalina na sheria hiyo na liko tayari kuruhusu majengo ya makanisa yake kutumika kuwafungisha ndoa mashoga na wasagaji.

Hata hivyo kanisa la Church of England limetangaza kuwa halitaruhusu ndoa kama hizo kufanyika kwenye makanisa yao.

Chama cha siasa cha Liberal Democrats ndicho kilichoipigia kampeni sheria hiyo ili kutimiza ahadi za usawa walizozitoa wakati wa kampeni ambazo ziliwafanya wapate kura nyingi kiasi cha kuweza kuunda serikali ya mseto na chama cha Conservative Party.

Jumuiya za kiislamu na jumuiya za kanisa katoliki zimeendelea kusisitiza kuwa mafundisho yao yanasema kuwa ndoa ni kati ya mwanaume na mwanamke.



EU yaitaka Libya isiwabane waandamanaji





Umoja wa Ulaya umeutaka uongozi wa Libya kuwaruhusu raia wake kujieleza kwa uhuru baada ya machafuko ya jana usiku yaliyotokea mjini Benghazi na kutangazwa na vyombo vya habari nchini humo.Kulingana na taarifa za kituo cha televisheni cha taifa,kundi la kiasi ya watu 500 waliandamana nje ya afisi za serikali ili kuushinikiza uongozi kumuachia huru mwanaharakati mmoja kabla ya kuelekea kwenye uwanja ulio katikati ya mji mkuu.Duru zinaeleza kuwa purukushani zilitokea pale polisi na wafuasi wa serikali walipopambana na wanaharakati hao.Kwa mujibu wa mkurugenzi wa hospitali moja kwenye eneo hilo,watu 38 wakiwemo maafisa wa polisi walijeruhiwa na wakapewa matibabu kwenye hospitali hiyo.

Wakati huohuo Serikali ya Libya ilitangaza leo kuwa itawaachia huru kutoka gerezani wanaharakati 110 wakiislamu .






MuIraqi aliyetoa taarifa za silaha za maangamizi makubwa ajigamba



Raia mmoja wa Iraq aliyebainika kuwa na nafasi muhimu katika hali iliyochangia kuuhalalisha uvamizi wa Marekani nchini mwake mwaka 2003 anaripotiwa kuwa anajivunia kuwa chanzo cha kuvurugika kwa utawala wa Saddam Hussein.Hii leo,gazeti la Uingereza la,The Guardian-lilichapisha ripoti zinazoeleza kuwa Rafid Ahmed Alwan al-Janabi aliyepewa jina la Curveball na majasusi wa Marekani na Ujerumani waliokuwa wakikichunguza kisa hicho-ndiye aliyeeleza kuwa uongozi wa Saddam Hussein una silaha za maangamizi makubwa.Kulingana na gazeti hilo,Rafid al-Janabi anajigamba kuwa alipata fursa ya kusambaza uvumi uliochangia kuuondoa madarakani uongozi wa Saddam Hussein.Hata hivyo uchunguzi uliofanywa ulibaini kuwa hakukuwweko na silaha zozote za maangamizi nchini Iraq.

No comments:

Post a Comment