KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, February 19, 2011

Mauaji ya kimbari nchini Libya?



Kanali Gaddafi
Mabalozi wa Libya katika Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuingilia kati mzozo nchini humo ili kusimamisha vitendo vya uhalifu vinavyo tekelezwa dhidi ya waandamanaji.

Naibu balozi wa Libya katika umoja wa mataifa, Ibrahim Dabbashi, amesema, raia wa Libya lazima walindwe kutokana na kile alichokitaja kama mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na maafisa nchini humo.

Bw Dabbashi amesema hizi ni nyakati za mwisho za Kanali Gaddafi na kwamba ni lazima afunguliwe mashtaka.


Naye balozi wa Libya nchini Marekani, Ali Aujali, amesema hataendelea kuiwakilisha serikali yake.


Maandamano nchini Libya
Amesema utumiaji wa nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji hautakubalika.

Wakati huo huo, kanali Muammar Gaddafi amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu mzozo huo kuzuka, kupitia runinga ya taifa. Ripoti za awali zilikuwa zimedokeza kuwa huenda akatoa taarifa kamili kuhusu matatizo yanayoendelea, lakini alizungumza kwa chini ya dakika moja tu.

Bw Gaddafi alionekena akiwa ameketi ndani ya gari huku akiwa ameshikilia mwavuli na mlango wa gari ukiwa wazi.

Kiongozi huyo wa Libya alisema alikuwa akizungumza na vijana katika eneo la Green Square mjini Tripoli nyakati za jioni, na kuongeza kuwa anataka kuweka wazi kuwa niko mjini Tripoli wala sio nchini Venezuela.

No comments:

Post a Comment