KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, February 19, 2011

Kuna hatari ya kuibiwa kwa watoto Uwanja wa Sabasaba


ZAIDI ya watoto 80 wanaendela kusota katika uwanjaw a Sabasaba walipohifadhiwa ili wazazi wao waende kuwachukua mahali hapo.
Watoto hao ambao wamehamishwa kutoka Uwanja Wa Uhuru na kuhamishwa katika uwanja wa Sabasaba bado wazazi ama walezi hawajaonekana kuwachukua waondoke mahalai hapo.

Chama cha Msalaba Mwekundu kinaendelea kuwalea watoto hao na kuwa na hofu kubwa ya kuibiwa kwa watoto hao.

Hata hivyo chama hicho kimetoa masharti ya kuchukua watoto hao, endapo mtu atajitokeza kuchukua motto anatakiwa awe na alama yeyote itakayomuonyesha kuwa mtoto anayemuhitaji kuwa ni wake kiukweli.

Wamewataka kuwa na kama kitambulisho chochote ama kadi ya kliniki ya motto, picha yeyote ama alama nyingine yeyote itakayomtambulisha kama ni mtoto wake.

Jana zaidi ya watoto 500 waliokotwa sehemu mbalimbali za jiji wakiwa wameachwa na wazazi wao katika harakati za kuokoa uhai wao.

Watoto haow anaoanzia umri wa miezi sita na kuendelea.

No comments:

Post a Comment