KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Waziri wa Sudan Kusini auawa




Waziri mmoja kutoka serikali ya Sudan kusini ameuawa ndani ya jengo la wizara yake mjini Juba.

Philip Aguer wa jeshi la SPLM alisema, waziri wa maendeleo ya ushirika na masuala ya vijijini Jimmy Lemi Milla ameuliwa na aliyekuwa mfanyakazi wake .

Mtu huyo naye alimwuua mlinzi wa waziri huyo ambapo baadae kukamatwa.




Waziri wa Sudan Kusini Jimmy Lemi Milla


Tukio hilo linatokea siku chache tu baada ya matokeo ya kura za maoni kuthibitishwa kuwa Sudan Kusini itakuwa taifa jipya duniani ambapo litaidhinishwa rasmi Julai 9.

Takriban asilimia 99 ya raia wa Sudan kusini walipiga kura ya kujitenga katika kura za maoni zilizofanyika mwezi uliopita.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir alisema atakubali matokeo.

Maafisa wa chama tawala cha Sudan People's Liberation Movement (SPLM) wanaamini lengo la uyfatuliaji risasi uliotokea siku ya Jumatano ni la kibinafsi zaidi kuliko kisiasa.

Lakini mwandishi wa BBC Peter Martell wa Juba amesema ni wazi kuwa kuna changamoto za kiusalama wakati Sudan kusini inapoelekea kupata uhuru wake rasmi.

Mshtuko
Kanali Aguer alisema mshambuliaji alikuwa mfanyakazi wa waziri huyo na anaamini pia alikuwa na undugu naye.

Mwandishi wetu anasema Bw Milla alifika ofisini kwake iliyopo katikati ya mji kama kawaida yake.

Lakini mlinzi wake aliacha bunduki yake ndani ya gari ambapo mshambuliaji huyo alivunja dirisha la gari, akachukua silaha hiyo na kuingia ndani na kumfyatulia risasi waziri huyo.

Mwanzo iliripotiwa kuwa mshambuliaji huyo alijipiga risasi, lakini baadae ikafahamika kuwa amekamatwa na polisi.

Mwandishi wetu alisema kuna mshtuko mkubwa Juba kuwa ufaytuliaji risasi umeweza kufanyika katikati ya mji na kwenye eno muhimu la serikali.

Mauaji hayo pia yamepunguza kasi ya furaha iliyopo baada ya tangazo la kuthibitishwa kwa Sudan kusini kujitenga.

Milla aliwahi kuwa mfuasi wa chama tawala cha kaskazini, lakini baadae akahamia SPLM baada ya mwaka 2005,kufuatia makubaliano ya CPA kutiwa saini ya kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo miwili.

No comments:

Post a Comment