KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Waasi wadai kuhusika na mlipuko wa Urusi



Kiongozi wa wanamgambo wa kiislamu nchini Urusi, Doku Umarov, ameonkena kwenye video akisema kuwa ni yeye ndiye aliyeagiza kufanyika kwa shambulio la uwanja wa ndege wa Domodedovo mjini Moscow ambapo watu 36 waliuwawa.



Doku Umarov


Amesema watafanya mashambulio zaidi. "Tunao ndugu wengi ambao wako tayari kujitolea mhanga kwa nia ya kufuata matakwa ya Allah na kulipiza kisasi dhidi ya maadui wa Allah." alisema.



Maua kwenye uwanja wa ndege wa Moscow


Umarov pia alisema kuwa wanataka kuunda serikali yao itakayofuata sheria za Kiislamu kaskazini mwa nchi hiyo.

Bw Umarov ambaye ameamejitangaza kuwa kiongozi wa eneo hilo la kaskazini mwa nchi hiyo na ni mojawapo wa viongozi wa waasi wa Chechen


Doku Umarov


Aliwahi pia kuwa waziri wa usalama katika serikali ya Chechnia kati ya mwaka 1996 na 1999.

Doku Umarov alisema kuwa pia aliagiza mashambulio ya kujitolea mhanga ya mwezi Machi mwaka wa 2010, katika treni mjini Moscow, na shambulio la Novemba 2009.

No comments:

Post a Comment