KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Maelfu wajitokeza tena Misri

Maelfu ya wananchi wa Misri wamemiminika katika mitaa ya mji mkuu Cairo, na kuelekea katika eneo la wazi la Tahrir, wakitaka serikali ya rais Hosni Mubarak kuachia madaraka

Maelfu wamejitokeza Tahrir


Waandishi wa habari wanasema, haya ni maandamano makubwa zaidi kuonekana, tangu maandamano yaanze Januari 25.

Hatua hii inakuja licha ya tangazo la serikali la mipango ya kufanya mabadiliko ya utawala kwa njia ya amani.


Mkusanyiko wa watu Tahrir


Rais Mubarak amesema atasalia madarakani hadi wakati wa uchaguzi mwezi Septemba.

Katika eneo la Tahrir, jaribio la kutaka kukagua vitambulisho lililokuwa likifanywa na wanajeshi limeshindikana kutokana na idadi kubwa ya watu wanaojiunga katika mkusanyiko huo.


Hadi Septemba.... Rasi Mubarak


Waandishi wa habari wa BBC wanasema, ujumbe kwa utawala ni mfupi tu - kuna uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wananchi wa ngazi zote wa Misri, na jitihada za serikali kutafuta muafaka hazitoshi.

Wael Ghonim, mkurugenzi wa huduma ya mtandao wa internet ya Google, aliyekamatwa na kuzibwa uso wake na majeshi ya usalama kwa siku 12, alipokelewa kwa shangwe wakati akiingia eneo la Tahrir

No comments:

Post a Comment