MBUNGE wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge amenusurika kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kufanikiwa kulipa faini ya shilingi laki saba baada ya Mahakama kumtia hatiani.
Hukumu hiyo ilitolewa jana katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni baada ya mbunge huyo kupatikanda na hatia ya makosa matatu na kila moja alitakiwa atumikie kifungo cha mwaka mmoja kila kosa.
Hukumu hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kwey Lusema baada ya kupatikana na makosa matatu ya kusababisha vifo vya watu wawili, kuendesha gari kizembe ikiwemo na kuendesha gari bila kuwa na bima.
Hivyo Hakimu Kwey alimtaka mshitakwia huyo kutumikia kifungo cha miaka mitatu ambapo kila kosa atatumikia kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya shilingi laki saba papohapo.Vifijo na vigelegele vilitawala kwa ndugu na jamaa wa mbunge huyo na kukubali kulipa faini kumnusuru na kifungo hicho na kuitana pembezoni huku michango hiyo ikikusanywa na mke wa mshitakiwa na alionekana kuwa na furaha tele usoni mwake na kufanikiwa kuchangishana pesa na hatimaye waliwasilisha pesa hizo na kuondoka na ndugu yao huyo.

Hivyo kesi hiyo iliyodumu kwa muda mrefu jana ilifikia tamati baada ya kulipa faini hiyo hivyo kumfanya awe huru.
Hukumu hiyo ilionekana kuvutia watu wengi na kusababisha kuwa na umati wa watu mahakamani hapo kushuhudia hukumu ya mbunge huyo ambapo kila mmoja aliichukulia hukumu hiyo kwa mtazamo tofauti
No comments:
Post a Comment