KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 30, 2010

Volcano yalipuka Sumatra, Indonesia







Volcano ya Sumatra Indonesia

Volcano ya Sumatra Indonesia

Volcano kwenye kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia imelipuka kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mia nne, na kusababisha watu wasiopungua elfu kumi na mbili kukimbia makaazi yao.

Volcano ya Mlima Sinabung inatuma angani moshi mkubwa wenye rangi nyeusi, mawe na salfar kwa masafa ya mamia ya mita.

Mlipuko huo ulisababisha serikali ya Indonesia kutangaza hali ya hatari.

Wakulima walizungumzia jivu kubwa linaloangukia mazao kwenye mashamba yao.

Maafisa walisema wanaandaa mahema na chakula kwa watu ambao waliondoka kutoka eneo la hatari.

Lakini hadi sasa jivu la volcano hiyo halijatatiza usafiri wa anga kwenye uwanja wa ndege ulio karibu wa Medan katika kisiwa cha Sumatra.

Priyadi Kardono, afisa kutoka Idara ya Taifa ya Kusimamia Majanga nchini Indonesia aliambia BBC kuwa baadhi ya watu waliokimbia makaazi yao wameanza kurejea wakati volcano hiyo ikionekana kupungua.

Indonesia ni sehemu ya eneo la Asia-Pacific na ina maeneo karibu 129 ya volcano ambazo zinaweza kulipuka

No comments:

Post a Comment