KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, August 26, 2010
UN yachunguza madai ya ubakaji DRC
Umoja wa Mataifa unachunguza madai kwamba waasi wamewabaka zaidi ya wanawake 150 na watoto wa kiume katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mashambulio hayo yalifanyika kwa muda wa siku nne hatua maili chache kutoka kwa kambi ya Umoja wa Mataifa, Mmarekani mmoja anayefanya kazi na shirika la kutoa misaada na daktari raia wa Congo walisema.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anatuma wajumbe wawili nchini humo kusaidia kufanya uchunguzi mashariki mwa nchi hiyo.
Bwana Ban pia ametaka serikali ya Congo ichunguze mashambulio hayo.
Wafanyakazi wanaotoa misaada na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa walifahamu waasi walikuwa kwenye mji wa Luvungi na vijiji vilivyo karibu na mji huo huko mashariki mwa Congo siku moja baada ya mashambulio yalivyoanza Julai 30, shirika la kutoa misaada ya matibabu la International Medical Corps (IMC) lilisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment