KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, August 28, 2010

Taliban washambulia jeshi la NATO Afghanistan

Wapiganaji wa Taliban

Waasi 18 wameuwawa nchini Afghanistan walipojaribu kuvamia vituo viwili vya kijeshi mashariki mwa nchi.

Mashambulizi hayo yalianza wakati wa asubihi kwenye vituo vikubwa katika jimbo la Khost karibu na mpaka wa Pakistan.



Zaidi ya wapiganaji wa 50 wa kundi la Taliban walishiriki katika shambulizi hilo kulingana na duru za kadhaa nchini humo.



Wapiganaji wa Taliban walifyatua risasi na maguruneti lakini wakashindwa kupenyeza ukuta wa usalama unaotumiwa na vikosi vya kigeni kujihami.


Wanajeshi wa kigeni ikabidi waitishe ndege za helicopter ili kurudisha nyuma mashambulizi hayo ya waasi

Wanamgambo wengi waliuwawa wakati waliposhambulia kambi ya Salerno. Wanne walikuwa wakivalia nguo maalum zinazotumiwa na watu wanaojitoa mhanga.

Msemaji wa NATO alisema hakuna wanajeshi wa kigeni wala askari wa Afghanistan ambao waliuwawa katika shambulizi hilo.

Mashambulizi makali ya Taliban dhidi ya vikosi vya kigeni na jeshi la Afghanista si ya kawaida.

Washambuliaji wa kujitoa mhanga na wapiganaji wameanzisha mashambulizi kadhaa kama hayo kwenye vituo vya kijeshi nchini kote.


Mwezi December mwaka jana maafisa saba wa shirika la ujasusi la Marekani CIA waliuwawa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga katika kambi ya Chapman katika jimbo la Khost.

No comments:

Post a Comment