KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, August 10, 2010
Mvua kubwa yanyesha Afrika Magharibi
Msimu wa mvua Afrika Magharibi umeanza kwa kishindo. Mvua ya mawe makubwa kama mayai uliangamiza mazao katika maeneo ya kati ya Guinea na mvua kubwa isiyowahi kuonekana kwa kipindi cha miaka 50 imenyesha kaskazini mwa Chad katika jangwa la Sahara.
Wakaazi wamekua wakiuhama mji wa Kaskazini wa Faya-Largeau, ulio sehemu za miti na chemchemi katikati jangwani na wamepaswa kulala nje mchangani.
Ramani
Shirika la msalaba mwekundu linaarifu kuwa zaidi ya watu 800 wamepoteza makaazi yao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Shirika hilo pia linatoa mahema, shuka na vifaa vya kupikia nchini Ivory Coast ambako watu wamekufa katika maporomoko ya udongo.
Nchini Niger zaidi ya nyumba elfu moja zimeangamizwa na takriban watu zaidi ya elfu tano wameathirika.
Umoja wa Mataifa nchini Niger unasema zaidi ya mifugo elfu thelathini imeangamizwa na mizoga yao inaonekana ikielea katika maeneo kadhaa.
Tahadhari
Nchini Nigeria mafuriko ya hapa na pale yamesababisha takriban wakulima laki moja kupoteza mazao yao na nchini Ghana zaidi ya watu 40 wamekufa.
Matangi ya kusomba maji machafu yameangamizwa na vyoo kufurika.
Mashirika ya kukabiliana na majanga nchini Ghana yametoa onyo la tahadhari katika mikoa mitatu ya kaskazini kufuatia vina vya maji kuendelea kupanda kwenye mabwawa mawili katika nchi jirani ya Burkina Faso.
Serikali ya huko inasema takriban watu 14 wameuawa na wengi wanapaswa kulala katika mashule na majengo mengine ya umma.
Siku ya Jumatatu takriban watu 13 walikufa wakati nyumba moja iliposombwa na maporomoko ya udongo katika mji mkuu wa Sierra Leone Freetown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment