Marekani imesema ina wasiwasi mkubwa kuhusu kile inasema ni matukio yenye kuleta utata yanayogubika uchaguzi wa urais uliofanyika wiki hii nchini Rwanda.
Katika taarifa yake, msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa katika ikulu ya White House, Mike Hammer, alikosoa kusimamishwa kwa magazeti mawili kabla ya uchaguzi wa siku ya Jumatatu.
Pia alizungumzia tukio la kufukuzwa kwa mtafiti wa haki za binadamu, kupiga marufuku vyama viwili vya kisiasa kushiriki uchaguzi, pamoja na kutiwa mbaroni kwa waandishi wa habari.
Bw Hammer alisema demokrasia si uchaguzi pekee, bali kuruhusu sauti za walio wachache kusikika na kuheshimiwa.
No comments:
Post a Comment