Mazishi yake Godfrey Binaisa yamefuatia mvutano kati ya familia na serikali huku baadhi wakitaka azikwe katika makaburi maalum ya waliokuwa marais wa Uganda na wengine wakitaka azikwe nyumbani kwake.
Sababu zilizotolewa za kutozikwa katiba makaburi maalum ya marais wa Uganda ni madai kuwa hakuwa shujaa.Mvutano huo,ulisababisha kucheleweshwa kuzikwa kwake,hadi pale spika wa bunge alipotangaza kuwa marehemu atazikwa katika eneo la Natete.
Leo ni siku ya mapumziko nchini Uganda kwa heshima ya kumzika marehemu Godfrey Binaisa aliefariki Ijumaa iliopita akiwa na umri wa miaka 90.Alitawala kwa kipindi cha miezi 11,kutoka Juni 20 mwaka wa 1979 hadi Mei 12 mwezi wa 1980.
Marehemu atakumbukwa kama mtu aliechangia kutengenezwa katiba ya nchi ya mwaka 1967 iliopiga marufuku ufalme.Pia kama rais aliongoza kipindi kigumu.Vilevile atakumbukwa kama kiongozi aliyeoa mke wa asili ya kijapani akiwa na umri mkubwa wa miaka 84.
No comments:
Post a Comment