KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, August 10, 2010
Avunja jungu kwa kuvunjika mguu
MWANAMKE mmoja [jina kapuni] mkazi wa Yombo, mwishoni mwa wiki hii amejikuta akipata jeraha ambalo hakulitarajia kwa kuzidiwa na kinywaji baada ya kutoka sehemu za starehe kwa kudai kuwa alikwenda kuvunja jungu.
Mwanamke huyo ambaye kwa sasa, yuko zahanati binafsi akijitibia kidonda na kuteguka mguu baada ya kuingia kwenye shimo ambalo hakuliona wakati akirejea kwenye vunja jungu hilo .
Chanzo cha karibu kinachotoka ndani ya familia ya dada huyo, kilidai kuwa, mwanamke huyo siku ya jumapili alipomaliza kula chakula cha mchana, aliwaaga kuwa anakwenda kustareheka ikiwa ni pamoja na kuvunja jungu kama alivyodai kabla hajatoka nyumbani hapo.
“Jamani mwezi ndio huo umekaribia, ngoja leo nikavunje jungu, ‘ alidai dada huyo
Ilidaiwa kuwa majira ya saa kumi na moja jioni mwanamke huyo alijikoki na kueleka kuvunja jungu hilo kwa kuwa mwezi mtukufu ni mwezi wa toba na wengi wao humalizia madhambi yao kabla mwezi huo haujaanza.
Ilidaiwa dada huyo kwenye kuvunja jungu hilo alizidiwa na pombe na aliporejea karibu na maeneo ya nyumbani kwake aliweza kuingia kwenye shimo na kuweza kuteguka mguu na kujijeruhi vibaya kwa kuingia kwenye shimo lilikuwa refu kidogo.
Hivyo inadaiwa dada huyo alipelekwa zahanati ya karibu kwa matibabu hadi habari hii inaandikwa dada huyo bado hajaweza kutembea sawasawa kama inavyotakikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment