KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Friday, August 27, 2010
Arsenal yamsajili Squillaci
Sebastian Squillaci
Klabu ya Arsenal imekamilisha taratibu za kumsajili mlinzi wa kimataifa wa Ufaransa Sebastian Squillaci kutoka klabu ya Sevilla.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 30 mwishoni mwa wiki iliyopita aliwasili London ambako alipimwa afya yake siku ya Jumatatu katika uwanja wa Emirates.
Mlinzi huyo wa kati wa zamani wa klabu ya Lyon ya Ufaransa hatacheza mchezo wa Jumamosi wa ligi dhidi ya Blackburn, lakini anaruhusiwa kucheza michezo ya ligi kuwania ubingwa wa vilabu vya Ulaya.
Squillaci anaonekana ataisaidia ngome ya Arsenal wakati huu walinzi wakongwe Sol Campbell, William Gallas na Mikael Silvestre wakiwa wameondoka katika klabu hiyo.
Imelezwa Arsenal imempatia mkataba wa miaka mitatu, licha ya kawaida ya Wenger kuwapatia mkataba wa muda mfupi wachezaji waliovuka umri wa miaka 30.
Mlinzi huyo alijiunga na Sevilla akitokea klabu ya Les Gones miaka miwili iliyopita na aliomba asichezeshwe katika mchezo wa marudio kutafuta nafasi ya kushiriki hatua ya makundi wiki iliyopita kati ya Sevilla na Braga ili asikose aweze kuichezea Arsenal katika mashindano hayo.
Wakati huu mlinzi mwengine wa Arsenal Philippe Senderos akiwa amehamia Evarton, Wenger alimsajili mlinzi wa kati Laurent Koscienly, ambapo kwa sasa klabu hiyo itakuwa na hazina kubwa ya walinzi wa kati baada ya Djourou naye kupona kabisa.
Squillaci alikuwemo katika kikosi cha ajabu ajabu cha Ufaransa kilichoshiriki Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini na alicheza walipofungwa na wenyeji Bafana Bafana, hali iliyosababisha wamalize wa mwisho katika kundi lao.
Wakati alipokuwa majeruhi, aliweza kuanza kucheza mechi 14 za ligi kwa timu yake ya Sevilla msimu uliopita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment