KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 1, 2010

Malaria haikubaliki Tanzania



SERIKALI kupitia wizara ya Afya inatarajia kugawa vyandarua milioni 14.6 kwa wananchi wake bure vyenye viatilifu katika kila kaya Tanzania Bara ikiwa ni kukabiliana na mapambana dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Mkakati huo unatarajia kugawa vyandarua viwili kila kaya ili kukabliana na kutokomeza malaria ambayo kauli mbiu ni “ Malaria haikubaliki”

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Afya, Profesa David Mwakyusa, alipokuwa akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2010/11.

Waziri Mwakyusa alisema katika mwaka wa fedha wa 2009/10, serikali ilisambaza bure jumla ya vyandarua milioni tisa vyenye viatilifu kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa lengo la kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini.

Alisema katika kufanya hivyo itahakikisha kila kaya inapata vyandarua hivyo ili kuweza kutokomeza maradhi hayo nchini ambayo imeonekana kumaliza watu wengi.

KAtika zoezi hilo pia wakaguzi maalum watakuwepo kukagua matumizi sahihi katika kila kaya kama vinatumika ipasavyo

No comments:

Post a Comment