KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, July 3, 2010

Ghana yalenga kuweka historia


Ghana inalenga kuweka historia ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia itakapochuana na Uruguay kwenye nusu fainali katika uwanja wa Soccer City, mjini Johannesburg siku ya Ijumaa.

Cameroon ilifika hatua ya robo fainali mwaka 1990 na Senegal ikaiga mfano huo mwaka 2002.

Kocha wa Ghana Milovan Rajevac anasema shinikizo kubwa zinazotokana na Ghana kuwa timu pekee kutoka Afrika iliyosalia kwenye mashindano hazitawaathiri Black Stars kwenye mchuano wao dhidi ya Uruguay.

Nchini Afrika Kusini inakofanyika michuano hiyo ya Kombe la Dunia, chama tawala cha ANC kimewaomba wananchi wote kuvalia mavazi ya rangi za Ghana na kuishabikia.

Pia kumekuwa na pendekezo la Ghana kubadili jina la timu Black Stars na kuitwa The Black Stars of Afrika.

Rais wa chama cha soka cha Ghana Kwesi Nyantakyi anasema anatumainia kwamba ushindi wa Ghana utasaidia kuleta umoja katika bara la Afrika.

Ghana iliishinda Marekani mabao 2-1 ili kufuzu kwa robo fainali, matokeo yaliyoleta hamasa kubwa sana kote barani Afrika, hasa baada ya kuondolewa kwa timu zingine tano zilizokuwa zinaliwakilisha bara hilo.

Ghana itakuwa bila kiungo Andre Ayew ambaye alipata kadi mbili za njano kwenye michuano iliyopita na pia mlinzi Jonathan Mensah aliyeonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Marekani.

Sullay Muntari atatazamiwa kuchukua nafasi ya Ayew ilhali safu ya ulinzi itaimarishwa na John Mensah na Samuel Inkoom.

Asamoah Gyan na Kevin-Prince Boateng wameshapona majeraha ya iliyopita na wanatazamiwa kuisumbua ngome ya ulinzi ya Uruguay.

Mlinzi Diego Godin ana jeraha, lakini bila yeye Mauricio Victorino atatazamiwa kuwadhibiti Gyan na Boateng, kama alivyoonyesha kwenye mchezo dhidi ya Mexico.

Diego Forlan na Luis Suarez wako imara katika safu ya ushambuliaji ya Uruguay.

No comments:

Post a Comment