KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 29, 2010

Waliojitokeza kumuomba mtoto wakataliwa na uongozi wa hospitali


MWANAUME mmoja amejitokeza hospitali ya Amana iliyopo Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam kutaka apewe mtoto anayetunzwa hapo kwa kujitambulisha ni mzazi wa mtoto huyo na hakufanikiwa kupewa hadi kupatikane kwa uthibitisho wa kina
Mwanaume huyo amejitokeza hospitalini hapo jana asubuhi, akiongozana na watu wengine huku akijitambulisha kuwa ni baba wa mtoto huyo.

Mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Alphonce, mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatunzwa hospitalini hapo baada ya mama yake kufariki ghafla punde tu alipofikishwa hospitalini hapo akitokea katika kituo cha Afya cha Jeshi la Ulinzi Gongolamboto.

Mama wa mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Mikaela Mikael, alikufa siku kumi zilizopita na mtoto huyo kubaki hapo bila ndugu wa aina yoyote kujitokeza na hadi jana siku ya 11 baba huyo kujitokeza na kudai kuwa ni mtoto wake.

Hivyo walipofika na kuona uongozi husika hawakuruhusiwa kuchukua mtoto huyo na kutakiwa kurudi leo ili kuthibitisha uhalali wa undugu huo.

Wauguzi walisema kuwa mama huyo alipofikishwa hapo walipompima waligundua kuwa alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na baadae walianza kumuona mama huyo akizungumza maneno yasiyofahamika na kuanza kumtundukia madripu kumuongezea nguvu na alfajiri aliaga dunia.

Mwanaume huyo alijitokeza hospitalini hapo siku ya kumi na moja baada ya kuona taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari na kutaka apewe mwili wa marehemu na mtoto huyo.

Alipohojiwa na vyombo vya habari kuhusiana na tukio hilo alisema alikuwa anafahamu ugonjwa uliokuwa unamsumbua mwanamke huyo ni nguvu za giza na hakuwa na taarifa kama alifikishwa hospitalini kwa kuwa jirani yake alimchukua na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji.

Hivyo alishtuka kuona taarifa hizo kwenye vyombo vya habari baada ya mwanamke huyo kutoonekana kwa ndugu zake kuuchukua mwili wa marehemu na mtoto huyo akiwa anatunzwa wodini.

No comments:

Post a Comment