KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 29, 2010

Uingereza kupunguza idadi ya wahamiaji


Wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza, kwa mara ya kwanza imeweka kikwazo kuhusu idadi ya wahamiaji kutoka nje ya Umoja wa Ulaya watakaoruhusiwa kuingia nchini humo.

Waziri wa mambo ya ndani,Theresa May amesema hatua hiyo ni katika juhudi za kupunguza idadi ya wahamiaji hadi itakapofikia jinsi ilivyokuwa miaka ya tisini.

Ni wafanyikazi elfu ishirini na nne pekee kutoka nje ya Umoja wa Ulaya watakaoruhusiwa kuingia nchini Uingereza kati ya sasa na mwezi Aprili, mwaka ujao ambapo serikali inapanga kuanzisha sheria mpya ya kudhibiti wahamiaji.

Serikali bado haijasema sheria hiyo mpya inalenga kupunguza idadi ya wahamiji kwa kiwango gani.

Idadi ya wahamiaji nchini Uingereza imeripotiwa kuongezeka kwa kasi zaidi katika miaka ya hivi karibuni.

Hatahivyo,hatua ya serikali ya Uingereza kupunguza idadi ya wahamiaji haijashabikiwa na viongozi wa kibiashara na kisiasa, ambao wameikosoa vikali, wakisema itaathiri uchumi wa nchi na haitachangia kwa njia yoyote katika kupunguza wahamiaji haramu.

Wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni,kura ya maoni ilionyesha kuwa uhamiaji na uchumi ndiyo yalikuwa maswala muhimu zaidi kwa wapigaji kura, huku wengi wao wakilalamika kuwa idadi ya wahamiaji imeongezeka sana.

No comments:

Post a Comment