Ingabire: Wafuasi wake ni miongoni mwa waliokamatwa
Polisi nchini Rwanda wanamzuilia kiongozi wa chama cha upinzani cha PS Imberakuri, Bernard Ntaganda kwa madai ya uchochezi na kubuni chama cha waasi.
Hii ni baada ya Rais Paul Kagame kuzungumzia jaribio la kufanyika maandamano hapo jana, wakati tume ya uchaguzi nchini humo ilipoanza kupokea majina ya watu wanaotaka kugombea kiti cha urais utakaofanyika mwezi wa nane.
Rais Kagame anasema wahusika lazima wafuate sheria lakini upande wa upinzani unadai kuwa vyombo vya dola vinawabana.
Msemaji wa polisi Eric Kayiranga, amethibitisha kukamatwa kwa Bernard Ntaganda, lakini amesema bado haja funguliwa mashtaka.
Kiongozi mwingine wa Upinzani Victoire Ingabire amesema wajumbe wa chama chake cha United Democratic Forces walikamatwa wakati wa maandamano mjini Kigali.
No comments:
Post a Comment