KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Tuesday, June 29, 2010
Oprah Winfrey, atisha kwa utajiri
Mtangazaji wa televisheni Marekani Oprah Winfrey ametajwa kuwa mtu mwenye mvuto na utajiri mkubwa duniani kupitia jarida la Forbes.
Winfrey amempiku muigizaji wa filamu Angelina Jolie kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya watu 100 mashuhuri kwa mwaka katika jarida la Forbes.
Nafasi hizo hupangwa kutokana na mapato ya mtu na kiwango anachoonekana kwenye vyombo vya habari.
Muimbaji Beyonce, amechukua nafasi ya pili, huku mkurugenzi wa filamu James Cameron akiingia tena kwenye chati na kuchukua nafasi ya tatu kufuatia mafanikio yake ya filamu ya Avatar.
Lady Gaga amepanda katika nafasi mpya ya orodha hizo akiwa nafasi ya nne.
Kama ilivyo kwa Beyonce, mapato yake na taarifa za maisha yake kwa ufupi zimeongezeka katika miaka 12 iliyopita kutokana na ziara zake duniani na mikataba mbalimbali.
Jolie, wakati huo huo, ameteleza kutoka nafasi ya juu hadi kufikia nafasi ya 18.
Nyota wa gofu aliyezingirwa na matatizo mengi Tiger Woods ni nyota pekee wa michezo kuwa katika 10 bora.
Simon Cowell
Simon Cowell
Britney Spears amekuwa wa sita, ikufuatiwa na U2 kwenye nafasi ya saba, wakiwa wamerudi katika 100 bora.
Sandra Bullock, aliyeshinda tuzo ya Oscar mwaka huu ya muigizaji bora wa kike, amepanda chati kwa kasi kutoka nafasi ya 92 hadi kufikia ya nane.
Johnny Depp naye amerudi kwenye chati katika nafasi ya tisa.
Kigogo wa muziki Simon Cowell ameongoza kwa upande wa Uingereza, kwa kupanda nafasi 14 hadi kufikia nambari 11.
Lakini Clodplay imeshuka kwa nafasi 20 na kuwa ya 35 katika mwaka ambao bendi hiyo imepumzika kufanya ziara na kuamua kurejea studio.
Nyota wa Harry Potter Daniel Radcliffe ameshika nafasi ya 82.
Umaarufu wa mfululizo wa Twilight ulionekana kwa kuwepo muigizaji wa kike Kirsten Stewart akiwa nafasi ya 66 na Robert Pattinson nafasi ya 50, wote wakiwa kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza.
Mwaka huu, Forbes iliongeza kigezo cha mtu maarufu kuwepo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook au Twitter, pamoja na mapato na kiwango cha kuonekana kupitia vyombo vya habari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment