KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, June 24, 2010
Mahabusu kushiriki kura ya katiba Kenya
Jopo la majaji watano wa mahakama ya kusuluhisha mizozo ya kikatiba limeamuru kuwa wafungwa wote nchini Kenya wapewe haki ya kushiriki katika kura ya maoni kuhusu katiba mpya mwezi Agosti.
Agizo hilo limetolewa baada ya ombi lililowasilishwa na wafungwa katika gereza moja mjini Mombasa wakidai walikuwa na haki ya msingi kushiriki katika kura hiyo.
Wakikubaliana na wafungwa hao, majaji hao wameipa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya siku 21 kuwasajili mahabusu hao kama wapiga kura. Ili kuwawezesha wafungwa hao kupiga kura, mahakama hiyo ya kikatiba imeamuru kuwa jela zote nchini Kenya ziwe vituo vya kupigia kura wakati wa kura hiyo ya maoni.
Katiba ya Kenya kwa sasa hairuhusu wafungwa kushiriki katika uchaguzi na hivyo basi uamuzi uliotolewa na mahakama ya kikatiba utatumika tu katika kura ya maoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment