KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Azamia Jela Baada ya Kuona Maisha Magumu Uraiani


Mwanaume mmoja wa nchini Msumbiji ambaye alitoka jela kwa msamaha wa rais baada ya kukaa jela miaka mitano, amevunja ukuta wa fensi ya jela na kurudi gerazani baada ya kuona maisha ya uraiani ni magumu.
Camilo Antonio, 28, aliamua kurudi gerezani mwenyewe baada ya kugundua kuwa hayapendi tena maisha ya uraiani.

Camilo alitumikia miaka mitano jela kati ya 10 aliyohukumiwa kwa kumuua baba yake wa kambo, alitolewa jela baada ya kupewa msamaha wa rais.

Camilo ambaye alitumikia kifungo chake katika jela ya Manica iliyopo ukanda wa kati wa Msumbiji, alishindwa kustahamili maisha magumu ya uraiani na kuamua ni bora arudi jela.

Alishindwa kupata kazi na alikuwa na hofu familia ya baba yake wa kambo ingejaribu kumuua.

Camilo aliamua kuvunja sehemu ya ukuta wa jela ili aweze kuingia ndani. Alikamatwa na kushtakiwa kwa uharibifu wa mali za serikali na alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja.

"Kwajinsi ninavyoona jela kwangu ni sehemu salama kuliko sehemu zote", alisema Camilo kuliambia gazeti la Noticias la nchini Msumbiji.

"Sitaki kuishi jela maisha yangu yote lakini kwa wakati huu jela ni bora kuliko sehemu yoyote ile", alimalizia kusema Camilo.

No comments:

Post a Comment