KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 3, 2010

Sekta ya elimu nchini Kenya kuchunguzwa




Wachunguzi watakagua mahesabu kati ya mwaka 2003 mpaka 2007.
Uchunguzi mpya umeanzishwa nchini Kenya kukabiliana na madai ya rushwa katika sekta ya elimu. Uchunguzi utaangazia kipindi cha kati ya mwaka 2003 na 2007.

Gazeti la Daily Nation la nchini humo limesema wachunguzi watakagua kumbukumbu za mahesabu ya shule takriban 20,000 sawa na asilimia 75 ya shule zote na pia watawakagua maafisa.

Daily Nation limesema uchunguzi uliofanywa katika miezi iliyopita, umefichua hasara ya zaidi ya dola milioni zilizotengwa kwa mpango wa mafunzo ya walimu.

Lakini ripoti hiyo inasema uchunguzi mpya utaangazia zaidi kilichotokea kuhusu fedha za wahisani zilizotolewa kusaidia sekta ya elimu Kenya kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Inaeleza kuwa wakaguzi wa mahesabu 220 watashiriki katika shughuli hiyo. Pia watachunguza kwa karibu shule ambazo zilitengewa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mapya.

No comments:

Post a Comment