KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, March 6, 2010
Mamilioni ya watoto kupata chanjo ya polio barani Africa
Kampeni za kutokomeza maradhi ya kupooza au polio katika mataifa ya magharibi na kati kati mwa bara la Afrika zinaanza leo, zikilenga watoto wapatao millioni thamanini na tano.
Wafanyakazi wa huduma za afya na watu waliojitolea watakwenda nyumba hadi nyumba katika nchi kumi na tisa, na kuwapatia chanjo kupitia mdomoni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.
Bara la Afrika limepiga hatua kubwa katika miaka ya hivi karibuni katika kupambana na mardhi hayo ya kupooza, ambayo kwa kawaida huathiri mfumo wa neva mwilini, lakini baado haujaweza kutokomezwa kabisa.
Juhudi za huko nyuma za kuangamiza ugonjwa huo zilishindikana kwa sababu watoto wengi hawakuweza kupatiwa chanjo.
Baadhi ya viongozi wa kidini nchini Nigeria pia walipinga kampeni za kutoa chanjo hiyo, wakidai kuwa zilikuwa ni njama za mataifa ya magharibi kutaka kusambaza virusi vya HIV na ugumba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment