KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, March 6, 2010
Ethiopia yakanusha ripoti ya BBC
Ethiopia yakanusha ripoti ya BBC
Mashirika ya misaada na serikali ya Ethiopia zimekanusha madai ya matumizi mabaya ya fedha katika ripoti iliyotolewa na BBC.
Katika ripoti hiyo BBC imesema uchunguzi wake umegundua mamilioni ya fedha za msaada kusaidia waathiriwa wa janga la ukame miaka ya thamanini zilitumika kununua silaha.
Abadi Zemo, afisa mwandamizi wa muungano wa vyama unaotawala Ethiopia, amesema madai hayo hayana msingi wowote.
Pia alikanusha madai kuwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi, wakati huo aliamuru asilimia tano pekee za fedha hizo za msaada zitumike kukabiliana na ukame.
Naye nyota wa muziki wa rock, Bob Geldof, aliyeongoza juhudi za kukusanya kiasi kikubwa cha fedha hizo za msaada, amesema ripoti hiyo ni upuuzi mtupu.
Makundi ya waasi wa zamani yaliyohusika na usambazaji misaada maeneo waliyoyashikilia, wameiambia BBC ni asilimia tano tu ya fedha za msaada ndizo zilitumika kukabiliana na baa la njaa.
Uchunguzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA wakati huo ulisema kwa hakika msaada ulitumika kwa shughuli za kijeshi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment