KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, March 6, 2010
Brown: Mapema kuondoa vikwazo Zimbabwe
Brown: Mapema kuondoa vikwazo Zimbabwe
Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema vikwazo dhidi ya Zimbabwe ni lazima viendelee hadi masuala ya ukiukwaji haki za binadamu na vizuizi kwa vyombo vya habari viondolewe.
Baada ya mazungungumzo na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Bw Brown amesema Zimbabwe ni lazima ioneshe msimamo dhabiti wa kufanya uchaguzi huru na wa haki kwa siku zijazo.
Rais Zuma, akiwa katika ziara ya kiserikali nchini Uingereza, ameshauri vikwazo viondolewe ili kuisaidia Zimbabwe kupiga "hatua mbele."
Waziri Mkuu Brown pia amepongeza maandalizi ya Kombe la Dunia yanavyokwenda nchini Afrika Kusini.
Ameitaka Afrika Kusini kutumia "msukumo na vuguvugu" la mashindano hayo kuhakikisha kila mtoto nchini humo anapata nafasi ya kwenda shule ya msingi.
Wakati wa mazungumzo hayo mjini London, viongozi hao wawili walijadili masuala mbali mbali yakiwemo uchumi duniani, uhusiano wa biashara, mabadiliko ya hali ya hewa na suala la kuenea kwa nuklia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment