KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Saturday, February 6, 2010
Wanajeshi Burundi watuhumiwa kwa uasi
Wanajeshi 33 wa Burundi wanaotuhumiwa kuhusika na uasi wakati wakiwa katika jeshi la kutunza amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia wamefikishwa mahakamani.
Wanashtakiwa kwa kukataa kutii amri mwezi Januari 2009 wakipinga suala la kutolipwa mishahara.
Waendesha mashitaka wamesema wanajeshi hao walibeba silaha bila ya idhini, wakiwashutumu maafisa kuwaibia fedha zao.
Burundi na Uganda ni nchi pekee zilizopeleka majeshi yake Somalia katika jeshi la Umoja wa Afrika.
Wakifanya kazi na serikali ya mpito ya Somalia iliyo dhaifu, wanajeshi hao wanashikilia maeneo machache muhimu mjini Mogadishu.
Pia hukabiliana na mashambulio ya mara kwa mara kutoka kwa wapiganaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment