KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, February 1, 2010

Waingereza waliotekwa waomba msaada

Waingereza wawili waliotekwa na maharamia wa kisomali wamesema wanahitaji msaada wa dharura kutoka kwa serikali ya Uingereza ili kutimiza madai ya kikombozi.

Rachel Chandler amemwambia mwandishi wa habari wa shirika la AFP, "hatuna muda wa kutosha na tunadhulumiwa."

Rachel na Paul Chandler kutoka Tunbridge Wells, Kent, walitekwa wakati wakielekea na mashua yao nchini Tanzania tarehe 23 Oktoba.

Maharamia wametishia kuwaua iwapo hawatolipwa kikombozi wanachodai.

Taarifa za hivi karibuni kuhusu hali ya Chandler na mkewe zilipatikana baada ya daktari kuruhusiwa kuwafanyia uchunguzi wa afya zao siku ya Alhamis.

Mpiga picha wa shirika hilo la AFP aliruhusiwa kuandamana nao

No comments:

Post a Comment