KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, February 6, 2010

Mwanawe Charles Taylor aamrishwa kulipa fidia

Jaji mmoja nchini Marekani amemuamuru mtoto wa kiongozi wa zamani wa Liberia , Charles Taylor, kulipa dola millioni ishirini na mbili kama fidia kwa raia watano wa Liberia walioteswa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Fedha hizo za fidia ziliamriwa kutokana na mateso waliyoyapata raia hao, mikononi mwa kundi la kijeshi lililo-ongozwa na Charles McArthur Emmanuel ambaye kwa sasa ni raia wa Marekani.


Waandishi wa habari wanasema haijabainika iwapo ana akiba ya fedha za kutosha kulipa fedha hizo za fidia.

Mwaka uliopita, mahakama ya makosa ya jinai nchini Marekani ilitoa adhabu ya kifungo cha miaka 97 jela kwa Emmanuel ambaye ni raia wa Marekani kwa kuhusika na mateso na mauaji ya watu nchini Liberia.

Mwaka uliopita, mahakama ya makosa ya jinai nchini Marekani, iliimpa Bw. Emmanuel adhabu ya kifungo cha miaka 97 gerezani kwa kuhusika na mateso na mauaji ya watu nchini Liberia.

No comments:

Post a Comment