
Marekani inasema imesikitishwa sana na uamuzi wa mahakama ya london ambao umeilazimisha serikali ya Uingereza kufichua taarifa za kijasusi kuhusu kuteswa kwa raia wa Uingereza.
Raia huyo Binyam Mohammed, amesema alitishwa na kulazimishwa kutolala alipokuwa katika kizuizi cha Marekani nchini Pakistan.

Afisa mkuu wa Marekani amesema hatua hiyo itaathiri ushirikiano wa kijasusi kati ya Marekani na Uingereza.
Taarifa hizo zilitolewa na Idara ya ujasusi nchini Uingereza, MI5. Mahakama ya London ilisema taarifa hizo zilipaswa kufichuliwa kwa kuwa baadhi yazo tayari zilikuwa zimefichuliwa kwa umma nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment