KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, February 9, 2010

Daktari wa Michael Jackson, Conrad Murray alifikishwa katika mahakama mjini Los Angeles


Daktari wa Michael Jackson kizimbani

Daktari wa Michael Jackson, Conrad Murray alifikishwa katika mahakama mjini Los Angeles na kushtakiwa kwa kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo miezi saba iliyopita.
Murray alikuwa ameajiriwa kumsaidia Michael Jackson kujiandaa kwa tamasha kadhaa mjini London na inaaminiwa kuwa alikuwa mtu wa mwisho kumwona mwanamuziki huyo akiwa hai.

Inadaiwa kuwa daktari Murray aliwaeleza wapepelezi kuwa alimpa Jackson dawa kadhaa ikiwemo ile yenye nguvu nyingi ya Propofol ambayo kwa kawaida hutumika hospitalini pekee.

Inadaiwa baada ya kumpa dawa hiyo Murray aliondoka kwa muda mfupi kutoka chumbani mwa Jackson ili kupokea simu na aliporudi akampata mwanamuziki huyo hapumui.

Afisa wa upelelezi alimpata daktari huyo na hatia ya kumpa Michael Jackson propofol kwa kupita kiasi kilichostahili na hivyo kusababisha kifo chake. Lakini alipofikishwa mahakamani kwa kosa hilo ambalo linaweza kumpa kifungo cha miaka 4 gerezani, Daktari Murray alisisitiza kuwa hakuna na hatia.

Daktari Murray aliachiliwa kwa dhamana ya dola 75,000 akisubiri kusikilizwa kwa kesi yake mwezi april

No comments:

Post a Comment