KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, February 20, 2010

Annan awaasa Kibaki na Raila




Kundi la viongozi mashuhuri wa Muungano wa Afrika limeelezea wasiwasi wake kuhusu mzozo wa kisiasa unaoendelea nchini Kenya, na kusema kuwa huenda ukaathiri utekelezwaji wa mkataba wa kitaifa wa serikali ya muungano.
Katika taarifa yao, kundi hilo linalo-ongozwa na aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa na mpatanishi mkuu katika mzozo nchini Kenya, Kofi Annan, limewataka rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga wafanye mashauriano ili kuutatua mzozo huo.

Mvutano wa hivi punde kati ya Rais Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga ulianza siku ya jumaapili, wakati Bw Kibaki alipobatilisha uamuzi wa awali wa Bw Odinga wa kuwasimamisha kazi mawaziri wawili waliohusishwa na kashfa za ufisadi.

Kufuatia hatua hiyo, Bw Odinga alitoa wito kwa Bw Annan kuja kuutatua mzozo huo.

Lakini taarifa ya jopo hilo la watu mashuhuri imemnukuu Bw Annan akitoa wito kwa waakilishi wa pande mbili walioshiriki katika kubuni mwafaka wa serikali ya muungano kutilia mkazo kutekeleza ajenda za mwafaka huo.

Jopo hilo limeelezea wasi wasi kwamba huenda mzozo uliopo ukatatiza juhudi za kupambana na ufisadi katika serikali ya Kenya.

Awali Rais Kibaki alisema hakuna mzozo wowote katika serikali ya Kenya.

No comments:

Post a Comment