KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, February 1, 2010

Al-Shabab waungana na al-Qaeda




Wapiganaji wa kisomali wa kundi la al-Shabab wamethibitisha kwa mara ya kwanza kuwa wapiganaji wake wanashirikiana na mtandao wa al-Qaeda.

Katika taarifa iliyotolewa na kundi hilo "Jihad ya pembe mwa Afrika lazima iungane na jihad ya kimataifa inayoongozwa na mtandao wa al-Qaeda".

Wakati huo huo, idadi kubwa ya watu wamefariki dunia katika mapigano mjini Mogadishu baada ya majeshi ya serikali kuvamia vituo vya wapiganaji.

Wapiganaji wa kiislamu wanadhibiti eneo kubwa Somalia ya kusini na kati.

Serikali ya Somalia, inayoungwa mkono na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, inadhibiti sehemu ndogo ya Mogadishu.

Licha ya kushutumiwa mara kwa mara na Marekani, hivi karibuni katika mahojiano na BBC al-Shabab lilikana kuwa na mahusiano na al-Qaeda

No comments:

Post a Comment