KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 20, 2010

Waziri wa Uhamiaji wa Kenya, Otieno Kajwang, ametoa onyo kwa wanasiasa kutoka nchi jirani ya Somalia


Kenya yawaonya wanasiasa wa Somalia waliotorokea huko

Waziri wa Uhamiaji wa Kenya, Otieno Kajwang, ametoa onyo kwa wanasiasa kutoka nchi jirani ya Somalia wanaotafuta hifadhi nchini humo, warudi nyumbani au wakae katika kambi za wakimbizi zilizoko nchini humo.

Bw Kajwang amesema kuwa wabunge wa Somalia hawapaswi kutumia Kenya kama eneo la kutafuta hifadhi kila wakati, wakati wameharibu taasisi nchini kwao.

Waziri huyo wa uhamiaji amewashutumu kuwa wanatumia mji wa Nairobi ambako wengi wametorokea kusababisha vurugu nchini Somalia, na kuleta matatizo nchini Kenya.

Takriban wabunge 530 wa serikali ya mpito ya Somalia wanaishi nchini Kenya.

Wabunge hao wanadai wamelazimika kuishi nje ya Somalia kutokana na kuwa hawajaweza kulipia ulinzi wao mjini Mogadishu.

No comments:

Post a Comment