KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 30, 2010

Marekani yajitetea kuiuzia silaha Taiwan




Marekani imetetea mpango wake wa kuiuzia silaha Taiwan baada ya China kuelezea kuwa imekasirishwa na mpango huo.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema siku ya Jumamosi kuwa, uuzaji huo wa silaha umesababishwa na hali ya usalama kati ya Taiwan na China.

China imetangaza hatua kadhaa dhidi ya Marekani katika kulipiza kisasi dhidi ya mpango huo wa silaha zenye thamani ya dola bilioni nne.

China imesema hatua hizo ni pamoja na kusitisha ubadilishanaji wa wanajeshi kati ya Marekani na China, kupitia upya masuala nyeti kati ya nchi hizo mbili na pia kuwekea vikwazo makampuni yanayouza silaha.

Naibu Waziri wa mambo ya kigeni wa China, He Yafei, alimwambia balozi wa Marekani, Jon Huntsman, kuwa mauzo hayo yanaweza kuwa na athari mbaya kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment