KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Monday, November 9, 2009
Wajerumani wakumbuka ukuta wa Berlin
Viongozi mbalimbali duniani wataungana na maelfu ya watu kuadhimisha miaka 20 tangu ukuta wa Berlin ulipoangushwa tukio lililomaliza vita baridi.
Sherehe kubwa zitafanyika katika lango la Brandenburg Gate - ikiwa ni alama ya kuunganika upya kwa Ujerumani mwaka 1990.
Ujerumani Mashariki iliyokuwa ikifuata siasa za Kikomunisti, ilijenga ukuta wenye urefu wa kilometa 155 mwaka 1961 kuizunguka na kuitenga na Berlin Magharibi.
Ukuta huo mzito uliwekwa kuwazuia watu kutoka iliyokuwa Ujerumani Mashariki kuukimbia ukomunisti.
Zaidi ya watu 100 inaaminika waliuawa eneo hilo la ukuta walipokuwa wakijaribu kutoroka.
Kikwazo hicho cha ukuta kiliondolewa bila kutazamiwa tarehe 9 mwezi wa Novemba mwaka 1989, baada ya kutokea wiki kadha za maandamano ya kupinga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment