KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, November 23, 2009

Viongozi 60 duniani waitikia Copenhagen


Idadi inaongezeka ya viongozi ambao wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kimataifa jijini Copenhagen kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na kuzua matumaini ya mafanikio.
Baadhi ya viongozi ambao wameonyesha nia ya kuelekea huko Denmark ni wale kutoka Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Uhispania, Australia, Japan, Indonesia na Brazil.

Haijulikani iwapo wenzao wa Marekani na Uchina watahudhuria.

Waakilishi kutoka nchi 192 wanatazamiwa kufika Copenhagen kujaribu kubuni mkataba mpya wa kudhibiti tabia nchi kuendeleza ule wa Kyoto uliozinduliwa mwaka 1997.

Hata hivyo kuna hofu ya kutopatikana kwa mwafaka wakati wa mkutano huo utakaoanza Desemba tarehe saba hadi 18.

Mwenyeji wa mkutano huo, Waziri Mkuu wa Denmark Lars Lokke Rasmussen alisema ili kupiga hatua, ni muhimu viongozi wa serikali kuhudhuria mkutano huo.

No comments:

Post a Comment