KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, November 18, 2009
Ronaldo tayari kuanza mazoezi
Cristiano Ronaldo huenda akaanza mazoezi kamili na timu yake ya Real Madrid siku ya Ijumaa akiwa amepona kiwiko cha mguu.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United aliumia walipocheza na Marseille tarehe 30 mwezi wa Septemba na amekosa michezo tisa kwa timu yake ya Real Madrid.
Baada ya kufanyiwa uchunguzi siku ya Jumanne ameruhusiwa kuanza mazoezi ingawa klabu yake haijatamka ni lini ataanza kucheza.
Afisa wa Madrid Emilio Butragueno, amesema wanahitaji kumchunguza kila siku na madaktari ndio wataamua.
Kuumia kwa Ronaldo pia kulimfanya akose kucheza michezo miwili ya timu yake ya taifa ya Ureno, kuwania kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Bosnia-Hercegovina.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment