KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, November 27, 2009

Ocampo aomba kupeleleza ghasia Kenya


Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa, Luis Moreno-Ocampo, anasema kuwa amewaomba majaji wa mahakama hiyo ruhusa ya kuanzisha upelelezi kuhusu ghasia za mwaka jana nchini Kenya baada ya uchaguzi mkuu.
Takriban watu elfu moja waliuawa katika ghasia hizo ziliozuka baada ya Rais Mwai Kibaki kutangazwa kuwa mshindi wa Uchaguzi mnamo Desemba mwaka 2007.

Upinzani ulidai kura ziliibiwa katika Uchaguzi huo.

Akizungumza na BBC Bw Ocampo amesema kuna sababu za kimsingi kuamini kwamba raia walitendewa maovu na vitendo vilivyokiuka haki za binadamu.

Kwa hiyo ikiwa majaji hao watalikubali ombi lake atakwenda Kenya kukusanya ushahidi kwa kuwasaili watuhumiwa na pia mashahidi na hapo ndipo wataamua kama kunastahili kufungua kesi ama la.

Ocampo alifafanua kuwa hawajibiki kutekeleza maelezo kuhusu orodha ya majina ya watuhumiwa ambayo ilikuwemo ndani ya bahasha aliyokabidhiwa mapema mwaka huu akisema hayo ni maoni ya wajumbe wa tume iliyochunguza mauaji hayo.

Yeye inampasa atoe uamuzi wake mwenyewe.

No comments:

Post a Comment