KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, November 11, 2009

Mdunguaji wa Washington auawa


Mtu aliyehusika na mauaji ya kudungua mwaka 2002 ndani ya mji wa Washington DC ameuawa baada ya rufaa yake kutupiliwa mbali.
Mawakili wa John Allen Muhammad wanasema alikuwa na maradhi ya akili,lakini gavana wa jimbo la Virginia Tim Kaine alikataa ombi lake la msamaha.




Jumatatu,mahakama ya juu zaidi marekani ilikataa rufaa yake ya kutaka kucheleweshwa kwa hukumu hiyo.

Muhammad, 48,aliuawa kwa sindano yenye sumu kali kwa kumuua Dean Harold Meyers,mmoja wa watu 10 waliouawa wakati huo.

Mshirikia wa Muhammad, Lee Boyd Malvo,aliyekuwa na miaka 17 wakati wa mashambulio hayo, alihukumiwa kifungo cha maisha jela.

No comments:

Post a Comment